Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BENKI ya maendeleo ya TIB imechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya taasisi za fedha za maendeleo ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa muda wa miaka miwili na kuhaidi ushirikiano pia amewataka watanzania kutumia fursa hiyo katika biashara na ushirikiano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya taasisi ya fedha za maendeleo za ukanda wa SADC Charles Singili amesema kuwa aliteuliwa nafasi hiyo mwezi Disemba mwaka jana na atahudumu nafasi hiyo kwa miaka miwili, kuanzia Disemba 2018 hadi Disemba 2020.

Singili amesema kuwa uteuzi huo ni muhimu kwa taifa na kwa benki ya maendeleo TIB pamoja na Serikali kwa ujumla na amewahimiza  wananchi kutumia fursa hiyo kwa kuwa kuna viongozi wanaoshikilia nafasi muhimu katika jumuiya ya SADC akiwemo Rais Dkt.John Magufuli ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa marais wa jumuiya hiyo na Agosti 2019 Rais Magufuli atashika usukani kama Mwenyekiti wa SADC pia Katibu mkuu wa sasa wa jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax ambaye  ni mtanzania pia.

Aidha Singili amesema kuwa hiyo ni nafasi pekee kwa Tanzania hivyo lazima majukumu yapokelewe na kuchapa kazi ili kuwa chachu ya maendeleo katika ukanda wa maendeleo kusini mwa Afrika. Aidha amesema kuwa Benki ya maendeleo TIB itatumia fursa hiyo kuhamasisha taasisi za fedha nchini na zile za nchi wanachama wa SADC katika kuhakikisha miradi ya maendeleo yenye maslahi ya kikanda inatekelezwa na hiyo ni pamoja na usafiri, nishati, maji na kuhakikisha fedha za kutosha zinapatikana.

Kuhusiana  fursa watakazozipa kipaumbele  Singili amesema kuwa watashirikiana na taasisi nyingine kwenye mtandao ili kuwezesha maandalizi ya miradi inayokopesheka kwa kutumia mfuko wa SADC wa kuandaa miradi mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Fedha za maendeleo za ukanda wa SADC Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uteuzi wa benki hiyo uliofanya Disemba mwaka jana pamoja na heshima iliyopata Benki hiyo kwa kuwekwa kwenye jedwali la heshima baada ya kupata daraja A katika masuala ya utawala bora na makundi ya uendeshaji tuzo iliyotolewa na taasisi ha AADFI, leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...