Mbunge wa jimbo la Segerea Bonnah Kamoli akikagua ujenzi wa barabara ya Kamungu kata ya Kiwalani, Minazi mirefu katika ziara ya  kukagua  miradi mbalimbali , leo jijini Dar es salaam.

* Asema sekta za elimu, afya, miundombinu ya maji na barabara itaendelea kupewa kipaumbele zaidi

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa jimbo la Segerea Bonnah Kamoli amefanya ziara na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni  ikiwa ni kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuhakikisha ahadi walizohaidi kwa wananchi zinatekelezwa kwa wakati na wananchi wa Segerea wanapata huduma bora zaidi.

Akiwa katika ziara hiyo  aliambatana na wajumbe wa kamati kuu ya halmashauri na Wilaya wa chama cha Mapinduzi amesema kuwa, lengo la kufanya ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo ambayo imekamilika pamoja na kuangalia namna miradi mingine ambayo inatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka huu inavyoendelea kutekelezwa.

Akiwa ziarani katika kata ya Kiwalani, Minazi mirefu Bonnah  amekagua ujenzi wa barabara ya Kamungu pamoja na soko la Migombani ambalo lipo katika hatua za awali za ujenzi na kusema kuwa pindi ujenzi wa barabara na soko hilo utakapokamilika wakazi wa eneo hilo watapata urahisi katika ufanyaji wa biashara zao, pia ametembelea soko la Kiwalani ambalo  linajengwa kisasa huku bajeti ya miradi hiyo ikifikia takribani shilingi bilioni 2.1 hadi kukamilika kwake ambapo Bonnah amemtaka mkandarasi anayesimamia miradi hiyo kuzingatia muda  aliopewa na ubora wa miradi hiyo.

Pia katika kata ya Kiwalani Mbunge Bonnah amekagua mradi wa ujenzi wa vyoo ambao umekamilika  katika shule za msingi Muungano na Bwawani ambapo ujenzi wa vyoo hivyo umegharimu shilingi milioni 19, na katika ukaguzi wa miradi hii Bonnah amesema:
“Ili wanafunzi waweza kufanya vizuri katika masomo yao lazima miundombinu iwe rafiki zaidi kwa watoto wetu, nitahakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao na kuwa viongozi bora wa baadaye.” Ameeleza Bonnah.

Akiwa katika  kata ya Kipawa Bonnah amekagua ujenzi wa barabara ya Karakata inayotokea Airpot ambayo hadi kufikia mwezi wa tatu ujenzi wake utakuwa umekamilika pamoja zahanati ya Kipawa miradi ambayo itagharimu takribani shilingi milioni 805 hadi kukamilika kwake na katika ukaguzi wa miradi hiyo Mbunge huyo amesema kuwa kuna miradi mingine inayoendelea ikiwemo ya maji (DAWASA) na hiyo yote ni katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi.

Vilevile Mbunge Bonnah ametembelea kata ya Kinyerezi, mtaa wa Kifuru ambapo amekagua ujenzi wa daraja linalofahamika kama  “Mwanzo mgumu” ambalo lipo katika hatua za mwisho katika kukamilika na limegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa kutoka katika mfuko wa jimbo, soko la Kinyerezi ambalo miundombinu ya vyoo na maji imekamilika na litaanza kutumika mara tuu baada ya sehemu iliyobaki kukamilika na mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 70.

Katika kuhitimisha ziara yake Mbunge huyo amekagua madarasa katika shule ya msingi Kinyerezi “A” mradi uliojengwa kupitia mfuko wa jimbo na nguvu kazi kutoka chama  cha jogging na umoja wa madereva pikipiki (bodaboda) kutoka vingunguti, mradi huo wa ujenzi wa madarasa 3 umegharimu zaidi ya shilingi milioni 50 huku pesa zaidi ikitarajiwa kuongezwa ili kujenga madarasa mengi zaidi ambayo misingi yake imekwisha jengwa. Akiwa shuleni hapo mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Shoo ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Mgufuli na Mbunge wao kwa ushirikiano bora wanaoutoa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2016, na kumwomba Mbunge Bonnah kuendelea na juhudi alizoanzisha hasa katika sekta elimu.

Akiongelea hali ya utekelezaji wa miradi hiyo Bonnah amesema kuwa miradi hiyo itakamilika kabla mwaka kumalizika na fedha kutoka katika mfuko wa jimbo zaidi ya shilingi milioni 70 zitawekezwa katika sekta ya elimu na miundombinu katika maeneo muhimu hasa hospitali na amesema kuwa kasi ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Mgufuli inaendana na mahitaji wa watanzania na ameahidi kuendelea kuongeza kasi katika kuleta maendeleo Segerea.
Mbunge wa Segerea,Bonnah Kamoli akizungumza na walimu wa shule ya msingi Kinyerezi A mara baada ya kukagua majengo yaliyojengwa kupitia mfuko wa jimbo, ambapo yamegharimu zaidi ya shilingi milioni 50 huku madarasa mengine yakiwa kwenye mpango wa kujengwa katika shule hiyo, leo jijini Dar es salaam.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinyerezi "A" Charles Shoo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mbunge Bonnah kukagua madarasa yaliyojengwa kupitia mfuko wa jimbo, Shoo ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa utendaji  hasa katika sekta ya elimu.
Mhandisi wa Wilaya ya Ilala anayesimamia utekelezaji miradi kata ya Kiwalani John Magori akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na miradi hiyo ambapo ameeleza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya miradi hiyo imekamilika na itagharimu shilingi Bilioni 2.9 na kueleza kuwa miradi hiyo itakamilika kama ilivyopangwa, leo jijini Dar es salaam.
Mafundi wakiendelea na ujenzi katika soko la Kiwalani, imeelezwa kuwa soko hilo linajengwa kisasa likiwa na sehemu za kuegesha magari na sehemu za kupimzika.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG)
Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli akizungumza na mafundi wanaojenga barabara ya Bethel Kiwalani, ambapo amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo, leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Emmanuel Massaka, MMG)
 Soko la Kiwalani likiwa katika hatua za ujenzi kama linavyoonekana pichani.
 Muonekano wa daraja lililo katika hatua za kukamilika, kata ya Kinyerezi mtaa wa Kifuru, wakazi wa eneo hilo wamemshukuru Mbunge wao kwa kufanikisha hilo kwani wamekuwa wakipata kero wakati wa mvua kutokana eneo hilo kujaa maji.
 Muonekano wa soko la Kinyerezi ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika, huku miundombinu ya vyoo na maji ikiwa imekamilika, leo jijini Dar es salaam.
 Muonekano wa madarasa ya shule ya msingi Kinyerezi A, ambayo yamekamilika kwa kuwezeshwa na mfuko wa jimbo ambapo zaidi ya shilingi milioni 50 zimetumika huku fedha zaidi zikitarajiwa kuongezwa ili kujenga madarasa ambayo msingi wake umekamilika, leo jijini Dar es salaam.
Muonekano wa vyoo katika shule za Kiwalani na Muungano mara baada ya kukamilika, mradi uliogharimu shilingi milioni 19.
Muonekano wa eneo ambalo soko la Migombani kata ya Kiwalani, Minazi mirefu litajengwa, wananchi ambao wameshalipwa fidia wakionekana wakihamisha mali zao ili kupisha ujenzi wa soko hilo, leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Emmanuel Massaka, MMG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...