NAIBU waziri wa mifugo na  uvuvi nchini Abdullah Ulega  amewataka wavuvi  nchini kutokuwa na hofu  katika shughuli zao za uvuaji wa samaki katika bahari maziwa  na mito.

Rai  hiyo ameitoa jana alipokuwa akizungumza na wavuvi wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani katika mwendelezo wa ziara zake nchini kwa kusudi la kuwaelimisha wavuvi kile  kinachofanywa na serikali  ya awamu ya tano.

Alisema kuwa serikali ilichukua hatua kali za kuchoma nyavu ambazo  zilikuwa ni hatari kwa kizazi  na masalia ya viumbe hao.

"Nendeni mkafanye kazi za uvuvi bila kuwa na wasiwasi  ila sheria  kanuni  na taratibu zifuate hakutokuwa na kiongozi wa aina yeyote ile atakayewasumbua "Alisema Ulega.

Aidha  aliongeza  kuwa kwa wale wote  waluochukuliwa jenereta zao taa za kuvulia zjmeamuliwa zirudishwe kwa wavuvi hao mara  moja kwani serikali imeamua virudishwe haraka sana,kuhusu faini  wanazopigwa wavuvi ni kwa mujibu wa she ria  za mazingira.

Mbali  na hayo  Ulega amewataka wavuvi hao kufanya kazi zao bila uoga  kwani kipindi hiki  cha hapa kazi tu  kimejikita katika kuhakikisha wananchi wake wanyonge  wanakuwa na kipato cha kati  ili kujiondoa katika umasikini.

Kwa upande  wake Juma Hassan mbaye ni mvuvi kutoka wilayani  Bagamoyo ameipongeza serikali kupitia naibu  waziri huyo kwa ufafanuzi mkubwa alioutoa kuhusu uvuvi haramu  ulivyokuwa ukididimiza maendeleo  ya taifa let kwa kipindi kirefu.

Naye mkuu wa wilaya hiyo  zainabu kawawa amewataka wananchi  kuwa na subra  kwani serikali  inayafanyia kazi malalamiko ya wavuvi na hasa  waliokamatiwa nyavu zao .
Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega akingalia baadhi   nyavu  hatari kwa kizazi  na masalia na viumbe hai zilizokamatwa katika maeneo mbalimbali ya  wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega akizungumza na wavuvi pamoja na wananchi wa kijiji cha Mligotini wilaya Bagamoyo mkoa wa Pwani.ambapo aliwaomba  kufanya kazi  bila kuwa na wasiwasi  ila sheria  kanuni  na taratibu zifuatwe,
 Semu ya sabuni pamoja na mafuta yanayo tengenezwa kwa zao la Mwani
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Zainabu Kawawa  akizungumza na wavuvi pamoja na wanchi wa wila hiyo  ambapo amewaomba  kuwa na subra  kwani serikali  inayafanyia kazi malalamiko ya wavuvi na hasa  waliokamatiwa nyavu zao .
Wavuvi pamoja na wanachi wa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani wakimsikiliza Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...