JK akiwa na Ruge Mutahaba wakati wa hafla ya miaka mitatu ya kituo cha kukuza vipaji nchini cha Tanzania House of Talents (THT)  usiku wa Desemba 8, 2009  katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Juu Ruge akiwa na nduguze. Chini akiwa na familia nzima ya Profesa na mama Mutahaba. Picha kwa hisani ya Nuru the Light

SWALI: Ruge mutahaba ni nani?

RUGE: Nimezaliwa Brooklyn,  New York,  Marekani,  mwaka 1970.


Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.

SWALI: Nini kilichotokea hadi ukajikuta uko clouds FM.

RUGE: Wakati nipo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo tuka-build good friendship. Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment. Hii ikazaa Clouds FM 88.4, ikazaa pia Prime Time Promotions iliyokuwa ina deal na matamasha ya muziki kuanzia Summer Jam ambayo baadaye ikawa Fiesta. Na pia ilihusika kuleta wanamuziki wote wa nje kuanzia kina Koffi (Olomide), Wenge BCBG, Chaka Khan, Sean Kingston,  Jay-Z na Beyonce, 50 Cents, Rick Ross, Buster Rhymes, Shaggy, Cabo Snoopy,  Davido, na wengine wote uwajuao wa kimataifa. Ni wengi kwa kweli. Afrika Mashariki na ya Kati hakuna aliyeweza na anayeweza kuleta wanamuziki nyota wa dunia kama Prime Time. 

SWALI: Tuambie kuhusu THT.

RUGE: Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri. Hivyo nikaona ni bora nianzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika.
Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kama Maunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...