"MATUKIO"
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

 

Na Mwandishi Wetu, Nairobi

Rais wa Kenya, William Ruto, amempongeza Jaji Mohammed Abdullahi Warsame baada ya kuapishwa rasmi kuwa jaji wa 14 wa Mahakama ya Juu ya Kenya, akieleza kuwa uzoefu wake mkubwa utasaidia kuimarisha utoaji wa haki nchini humo.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alisema ana imani kuwa Jaji Warsame ataleta mchango chanya katika mahakama hiyo ya juu kabisa nchini Kenya kupitia weledi na uzoefu wake wa muda mrefu katika sekta ya sheria.


 “Unaungwa mkono kikamilifu na tunakuombea mafanikio unapoanza jukumu hili muhimu la kulitumikia taifa letu,” alisema Ruto wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo.

Katika hafla hiyo pia, Rais Ruto aliwapongeza Evans Thiga Gaturu na Jedidah Wakonyo Waruhiu baada ya kutunukiwa hadhi ya Senior Counsel, akisema wameonyesha mchango mkubwa katika kuimarisha utawala wa sheria na demokrasia ya kikatiba nchini Kenya.

Ruto alisema Serikali ya Kenya itaendelea kushirikiana na mihimili mingine ya dola kuhakikisha haki inatendeka na mfumo wa sheria unaendelea kuimarika kwa manufaa ya wananchi wote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Rais wa Kenya, Kithure Kindiki pamoja na Jaji Mkuu na Rais wa Mahakama ya Juu Kenya, Martha Koome.

Na Mwandishi Wetu

Balozi Sita zinazowakilisha nchi zao nchini Tanzania zimeshiriki Tamasha la Piano ya muziki wa Franco Rhumba kwa ajili kupata furaha.

Akizingumza wakati kufungua Tamasha hilo lilofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Tanzania Jean Pierre Massala amesema kuwa Muziki huo unakuwatanisha kupata furaha pamoja na kujenga umoja .

Amesema kuwa kuwa waandaji wameweza kuona umuhimu kukaa pamoja na kupata furaha kupitia muziki huo ambao unapendwa na Wakongo na Jamii zingine.

Massala amesema kuwa matamasha hayo hayo ni muhimu kwani yanakutanisha watu tofauti ambao wanafanya kujenga umoja wenye furaha.

Kwa upande wa Balozi wa Morocco nchini Tanzania Zakaria El Goumiri. amesema kuwa wameshiriki Tamasha hilo kufurahi na kutaka waandaji waendelee kuandaa kwani linawaweka pamoja

Aidha amesema kuwa furaha za muziki za muziki zinaunganisha makundi mbalimbali kwa kuleta upendo

Mmoja wa waandaji Tamasha hilo Alain Izai amesema kuwa wanashukuru mwitikio walioupata katika Tamasha kwa kuungwa na Balozi Sita Kushiriki mwanzo hadi mwisho.

Izai amesema kuwa wataendelea kuandaa matamasha hayo mara kwa mara katika kutoa burdani kujenga furaha katika nyoyo zao.

Hata hivyo amesema Muziki wa Rhumba unapendwa na kila rika ambapo kazi yao ni kuendelea kutunga katika kuboresha nyimbo za muziki huo.


On August noon in forty-four, beneath Tanganyika’s sky,
In Mwazye’s quiet parish land, a child began to cry.
The sixth of nine, yet heaven-marked before the world could see,
A shepherd chosen long before he bent his first small knee.

His sister saw the spark in him and made a solemn vow,
To guard his dream with sacrifice, though trials pressed her brow.
Her youth she gave, her wages too, his schooling to defend,
So he might serve the Lord of Life until his journey’s end.

Through Karema’s halls and Kaengesa’s rising gleam,
Through Kipalapala’s sacred books and nights of ceaseless stream,
His mind grew luminous, his spirit ardent, his purpose living beam,
A leader formed by discipline, by prayer, by sacred theme.

Ordained a priest in seventy-one, still humble, still afraid,
Yet faithful to the call of God, whatever price was paid.
In Rome he drank from ancient wells of moral truth and grace,
Then hastened home to serve his land, not seek a higher place.

A bishop young in Nachingwea, in Tunduru he stood,
To build where little yet was formed, to plant where none yet could.
Though fear would knock upon his heart whenever roles were new,
His answer was obedience, God’s will he would pursue.

In Dar he rose to guide the flock where giants once had been,
A Cardinal in scarlet red, yet simple still within.
He asked, “Why beg for distant grain when ours can fill the bowl?”
And taught the Church to stand upright in dignity of soul.

From twenty parishes he dreamed of one hundred in their place,
They doubted such a vision vast could ever run that race.
But when he laid the crozier down and passed the charge along,
One hundred eighteen stood in faith, his vision proved them wrong.

For death to him was not defeat, nor darkness, nor despair,
But simply door to promised glory beyond all earthly care.
The pilgrim laid his labors down where saints and angels sing,
And entered joy no mortal tongue could fully name or bring.

Though on 19 February he left this earthly state,
On 28 February, in solemn farewell we congregate.
Not stripped of honor, nor lost to sight,
But clothed in dignity, in hallowed rite.

A priest for decades he faithfully stood,
A guide in truth, in strength, in good.
A bishop, archbishop, cardinal upright,
A conscience steady in nation’s sight.

Eternal rest, O Lord, bestow,
Let endless light upon him glow.
May he who led with faithful hand
Now dwell within God’s promised land.

And when the final trumpet rings,
And time surrenders all its kings,
May the shepherd, his flock, and the Church above,
Rejoice in resurrected love.

His spirit whispers still,
Through every heart he touched, through every faithful will.
Though tears may fall, his love will never fade,
A shepherd, father, guide, forever ours to aid.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


- The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.




Today, Tanzania celebrates a momentous milestone,
From Dar es Salaam to Dodoma, rails of progress are shown.
The Standard Gauge Railway, now electrified and new,
Marks a historic leap, connecting us through and through.

Leaders from all walks, gathered today,
Witnessing history, as tracks convey.
Opposition and ruling, side by side,
In this achievement, a national pride.

President Samia, with vision so clear,
Graces the launch, her presence dear.
Legacy carried with unshakable might,
Heralding a dawn, breaking the night.

Electrified pathways, a leap so great,
Connecting our regions, hand in hand.
Efficiency and speed, our journey redefined,
Economic tides, forever aligned.

Cargo moves swiftly, a trader’s delight,
Economies flourish, day into night.
Ten thousand tonnes, a train can bear,
Revolutionizing transport, beyond compare.

TRC’s Kadogosa, with pride declares,
Smooth operations, no unawares.
Safety and standards, we uphold,
In every journey, stories unfold.

Across borders, our vision extends,
Burundi and DRC, as trade ascends.
Intra-Africa bonds, we forge and mend,
A continental future, around the bend.

Makalla’s words, a patriotic call,
To guard our treasure, and stand tall.
Loans we’ve taken, for progress shown,
In every rail, our future grown.

From Dar es Salaam to Dodoma’s gate,
A new voyage begins, our collective fate.
A modern marvel, a nation’s pride,
On rails of progress, we boldly ride.

With progress and vision so bright and clear,
In 2025, my vote for Samia is near.
Her leadership shines, guiding us right,
For another term, she’s our shining light.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


- The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.


 

Na Seif Mangwangi Mbarali


KUNDI kubwa la zaidi ya Ng'ombe 500 na punda3 wamekamatwa na askari wa Jeshi Usu la  Uhifadhi katika hifadhi ya Taifa  Ruaha Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya huku wamiliki wa mifugo hiyo wakikimbia .

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, shirika la hifadhi za Taifa Tanzania na Mkuu wa hifadhi ya Ruaha, Goodwill Meng'ataki amesema mifugo hiyo imekamatwa katika eneo la ukwaheri ndani ya bonde Oevu la Ihefu.

Akizungumza katika eneo ambalo mifugo hiyo imehifadhiwa baada ya kukamatwa, Meng'ataki amesema eneo hilo ambalo mifugo hiyo imekamatwa ni  katikati ya hifadhi ya Ruaha katika bonde la Ihefu mahala ambapo ni chanzo cha maji ya mto Ruaha mkuu.

Amesema baada ya kukamatwa kwa mifugo hiyo, walifikisha suala hilo Polisi na baadae katika Mahakama ya Wilaya ya Mbarali na tayari Mahakama imeshatoa hukumu ya kutaifishwa kwa mifugo hiyo nakuagiza iuzwe.

"Kwa kawaida tunavyokamata mifugo ndani ya hifadhi, tunawasiliana na Polisi na kuifikisha Mahakamani. Tayari Mahakama imetolea maamuzi mifugo iliyokamatwa na imeagiza iuzwe, tunasubiri wanunuzi ambao tayari wako njiani kuja hapa Ukwaheri kwaajili ya kununua,"amesema.

Amesema wafugaji katika bonde la Ihefu katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha,  wamekuwa wabishi kuelewa katazo la kutochungia mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo na wamekuwa wakitumia mwanya wa eneo hilo kuwa na maji mengi kuingiza mifugo kwenye maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa na Askari wa Jeshi Usu la Uhifadhi.

" Kipindi hiki Kuna mvua nyingi zinanyesha ukanda huu, hawa wafugaji wamekuwa wakitumia mwanya huo huo kuingiza mifugo yao kwenye maeneo yenye maji mengi wakijua Askari wetu hawawezi kufika huko, lakini tunajitahidi kukabiliana nao,"amesema.

Amesema changamoto nyingine ni Askari wake kukabiliana na wafugaji ambao wamekuwa wakitumia silaha za jadi ikiwemo mishale na mikuki pindi wanapokamatiwa mifugo yao wakitaka kuitorosha.

Afisa Uhifadhi daraja la pili na Mkuu wa Kanda ya Usangu, Abisai  Nassari amesema baada ya kukamata mifugo hiyo 547 na punda 3,  walitumia msaada wa helkopta kuisogeza  hadi katika eneo lenye maji machache ndipo askari wake wakaisogeza hadi eneo la ukwaheri.

"Tunashukuru Serikali ya Rais Mama Samia kutuletea vifaa vichache vinavyotusaidia kupambana na mifugo na majangili wa wanyamapori, tunaomba kuongezewa  vifaa zaidi ili tuweze kufanyakazi yetu kwa ufanisi zaidi,"anasema.

Anasema changamoto kubwa wanayokabiliwa nayo ni namna ya kuwakabili wafugaji wanaoingiza mifugo katika bonde la Ihefu kwa kuwa eneo hilo ni chepechepe lililojaa matope kutokana na kuteremsha maji wakati wote.

Licha ya kundi kubwa kukamatwa na kutaifishwa, mwandishi wa habari hizi akiwa ndani ya Helkopta angani bado aliweza kushuhudia baadhi ya makundi makubwa ya ng'ombe wakiwa ndani ya eneo Oevu la Ihefu katika hifadhi ya Ruaha.


 


 

 



Usiku wa kuamkia leo Machi 28,2024 kumetokea ajali iliyohusisha mabasi mawili na roli la mafuta katika eneo la JKT Club karibu na Mlandizi mkoani Pwani.

Mabasi hayo ni Kampuni ya Sauli pamoja na New Force Taarifa zaidi za chanzo cha ajali hiyo na majeruhi zitatolewa baadaye leo na kamanda wa polisi. 

Endelea kutufuatilia kwenye page zetu Michuzi Tv, Michuzi blog kupata taarifa zaidi

Tumia Siku Yako ya Wapendanao kwa Njia ya Kipekee! Pata Mapumziko Maalum ya Valentine's Ndani ya Tanga Beach Resort! Tanga Beach Resort inakuletea ofa maalum ya siku ya wapendanao. Pata nafasi ya kufurahia mapumziko ya kifahari na kujivinjari na mpendwa wako. Tanga Beach Resort inakupa fursa ya kujenga upya mapenzi yako na kufurahia muda mzuri pamoja. Pata huduma bora za malazi, chakula, na burudani kwa bei nafuu. Jiunge nasi kwa siku ya wapendanao na ufurahie mapumziko yasiyosahaulika ndani ya Tanga Beach Resort!

 

Na Humphrey Shao,Michuzi TV

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto leo ameongeza zoezi la kujaza vifusi katika Barabara korofi za mitaa ya Vingunguti.

Akizungumza na Michuzi TV wakati wa zoezi hilo Meya Kumbilamoto amesema anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan ambaye amewezesha kutoa kiasi cha shilingi Milioni 360 zinazojenga soko jipya na la kisasa kwa Wafanyabiashara ndogo na Mama Lishe eneo la machinjioni.

"Ujio wa ujenzi huu ndio Neema kwetu kwani imewezesha kupatikana kwa vifusi hivi ambavyo vinasaidia kufukia Mashimo haya wakati tukisubiri Utekelezaji wa mradi mkubwa wa DMDP" Amesema Kumbilamoto.

Ameongeza kuwa anamshuku sana Mkurugenzi wa Halmashauri kwa moyo wake wa kujituma na kufanya kazi kwani ndani ya wiki tatu tu alizokaa katika Halmashauri hiyo ameweza kutatua changamoto nyingi ambazo zimekosa majawabu kwa muda mrefu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akisisitiza jambo kwa Watendaji na mafundi wanaojenga jengo la Wafanyabiashara ndogo Vingunguti.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akijadili Ramani na mafundi wanaojenga jengo Jipya la Wafanyabiashara ndogo na Mama lishe.
Mstahiki Meya wa Jiji la akisaidiana kuvunja jiwe na Vijana wa Vingunguti.



Na SALMA AMOUR, TANGA.

Wizara ya afya imefanya tafiti juu ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele yakiwemo Ngirimaji na Matende ambapo tafiti hizi zimebaini kuwa jumla ya halmashauri 119 hapa nchini kati ya 184 zina waathirika wengi wa magonjwa hayo huku jamii ikitajwa kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya sababu zinazopelekea kuongezeka kwa wagonjwa mbalimbali wengi hao wakiyahusisha na imani potofu.

Katika kuhakikisha kuwa magonjwa hayo yanapungua na kuyatokomezwa kabisa serikali imekuja na mikakati kabambe ya kutoa matibabu bure kwa wahanga ikiwemo upasuaji wa ngiri maji kote nchini mpango unaofadhiliwa na And Fund kutoka Uingereza ukiwa bado unaendelea kila mkoa hapa nchini unakilenga pia kuwafikia wagonjwa wengine elfu kumi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga walikoweka kambi ya siku tano kutoa huduma za upasuaji wa ngiri maji pamoja na dawa Daktari Faraja Liyamuya kutoka wizara ya afya katika mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele amesema kuwa kufwatia tafiti zilizofanyika katika halmashauri zote 184 zilibaini kuwa kati ya hizo ni halmashauri 119 ndizo zina maambukizi na vimelea vingi vya magonjwa hayo ikiwemo Ngiri maji na matende.

Amesema kuwa kumekuwa na nadharia tofauti zilizokuwa zimejengeka kwenye jamii kuwa magonjwa wa Ngiri maji na Matende yapo tu katika mikoa ya Pwani hali ambayo imekuwa ni tofauti baada ya tafiti zilizofanyika na kuweza kubaini kuwa mikoa yote nchini ina waathirika wa magonjwa hayo.

"Tulifanya tafiti katika halmashauri zote nchini 184 na kuona katika halmashauri 119 wapo watu ambao tayari walikuwa wameathirika au kuwa na vimelea na jitihada za kuhakikisha maambukizi hayaendelei katika halmashauri zote hizo zimeazaa matunda na sasa hivi bado tuna halmashauri tisa tu ndio ambazo bado tunaendelea kugawa dawa za kinga kwaajili ya kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha na kwa walioathirika wako katika halmashauri zote na kule ambako maambukizi yalionekana kuwa makubwa ndiko ambako tunao watu wengi waliopata madhara" alisema Dokta Faraja.

"Mpaka sasa hivi tangu tumeanza kambi hizi za upasuaji kwa Tanzania maeneo yote tumeshafanya upasuaji zaidi ya watu elfu kumi na tunakadiria wengine elfu kumi ambao bado wana uhitaji, na ugonjwa huu ulijengeka kuwa labda uko maeneo ya pwani peke yake kitu ambacho hakikuwa sahihi ukweli ni kwamba ugonjwa huu upo kila mahali ambapo kuna mbu wanaweza kueneza ugonjwa huu"

Aidha dokta Faraja alisema kuwa lengo la wizara kupitia mpango huo wa taifa wa kudhibiti magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele bado elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi kupitia njia mbalimbali hii ikilenga kuongeza uelewa na kuhamasisha wagonjwa kufika katika vitu vya afya zinakopatikana huduma hizo ili kupatiwa matibabu.

Kwa upande Wake Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Japhet Simeo ameleza kuwa tayari huduma hiyo ya upasuaji wa ngirimaji imeshafika katika wilaya za Pangani Muheza na Mkinga na wagonjwa elfu moja walishaifanyiwa upasuaji huku wakitarajia kuwafikia wengine 100 kwa siku tano ambazo kampeni hiyo inafanyika ndani ya jiji la Tanga.

"Katika mkoa huu wa Tanga maeneo ambayo tayari wameshapatiwa huduma ni Muheza Pangani na Mkinga na zaidi ya watu elfu moja wameshapatiwa huduma hii na tunatarajia kutoa huduma kwa watu wasiopungua mia moja baada ya kampeni tuliyoweka kwa siku hizi tano kutakuwa na vifaa ya kuweza kuhudumia watu mia tatu katika vituo vinne ambavyo ni kwenye halmashauri za Mkinga Pangani na Muheza " alisema Simeo.

Alisema kuwa tatizo la magonjwa ya Ngirimaji pamoja na yale ambayo hayapewi kipaumbele bado ni kubwa huku wagonjwa wakikabiliwa na unyanyapaa katika jamii huku wakijiapanga kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii pamoja na kuhamasisha wagonjwa kujitokeza katika vituo vya afya ili kuweza kupatiwa matibabu bure.

"Tatizo bado ni kubwa kwa jinsi ambavyo hawapewi kipaumbele na ukiangalia waliokwishapata huduma ni wale waliopata ujasiri wa kujitokeza kwenye matibabu kwahiyo inawezekana tatizo ni kubwa tofauti na tunavyoweza kuliona na tunaokutana nao, changamoto ya tatizo hili inaambatana na unyanyapaa kwa mgonjwa binafsi lakini jamii inaweza ikamnyanyapaa" aliongeza Ninashukuru sana serikali kwa hili kwa sababu hizi huduma ukizihitaji hospitalini gharama yake ni kubwa changamoto kubwa ni kuficha ugonjwa huu kwenye jamii unapoon watu mbele yako unakosa raha kabisa hasa nyumbani kunapokuwa na shughuli, naombeni sana jamik mwenye tatizo kama hili hii fursa tuitumieni vizuri tu" alisema Mashaka

Nae pia Ally Boza mgonjwa aliyesumbuliwa na ugonjwa wa Ngirimaji kwa muda wa miaka minne ameishukuru serikali kwa kupata huduma ya oparesheni bure akiiomba kuzidi kutoa elimuzidi huku akibainisha kuwa ugonjwa huo wengi katika jamii wamekuwa wakiuhusisha na imani potofu.

"Nina mwaka wa nne maradhi haya ninayo kiukweli wengi walikuwa wanasema ni uchawi lakini mimi niwaambie tu kwamba sio uchawi Ngirimaji ni maradhi kama maradhi mengine na inatibika kama kawaida ugonjwa huu wengi tulikuwa tunahitaji tupate huduma lakini uwezo hatuna , tunazidi sana kuishukuru serikali huduma n nzuri sana nahamasisha na wengineo waje" alisema Boza.

Kampeni hiyo ya kudhibiti magonjwa yasisyopewa kipaumbele ikiwemo Ngiri maji na Matende bado inaendelea nchi nzima kwa wagonjwa kujitokeza kayika vituo vya afya kufanyiwa upasuaji na kupatiwa dawa bure.

Dk Japhet Simeo mganga mkuu wa wa mkoa wa Tanga akizungumza na waandishi wa habari katika kituo Cha afya Mwakidila jijini Tanga
Daktari Faraja Liyamuya kutoka wizara ya afya katika mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga katika kituo Cha afya Mwakidila walipoweka Kambi ya siku Tano kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji kwa magonjwa ya ngiri MAJI


Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulishiriki katika maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.


NSSF ilitumia maonesho maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, matumizi ya mifumo ya TEHAMA kwa mwanachama na mwajiri ili kumrahisishia huduma bila kulazimika kufika katika ofisi za NSSF, kusikiliza na kutatua kero za wanachama na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo miradi ya nyumba za kisasa, miradi ya uwekezaji ya majengo ya Mzizima Tower na Mwanza pamoja na viwanja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Utalii Mwanza waliofika katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Festo Fute (wa pili kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Kahensa (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Hifadhi ya Jamii, Omary Mziya (wa kwanza kushoto) na Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Flora Ndutta (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya viongozi hao kutembelea Banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.








Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande, (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Flora Ndutta (kulia), kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko katika banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.

Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza Flora Ndutta (kushoto), akitoa huduma kwa wananchi waliofika katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza. (wa pili kushoto) ni, Mhasibu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Said Othman Mfuru.

Afisa TEHAMA wa NSSF, Janeth Bwire, akitoa maelezo kwa mwanachama jinsi ya kujihudumia kupitia simu yake kupitia mfumo wa WhatsApp chatbot. Huduma hiyo inapatikana kwa njia ya Whatsapp ambapo mwanachama halazimiki kufika Ofisi katika ofisi za NSSF. Elimu hiyo ya jinsi ya kutumia mifumo inatolewa katika banda la NSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.

Afisa Matekelezo Mwandamizi, sekta isiyo rasmi Diagi Janguo akimwandikisha Mwanachama mpya wa NSSF alipotembelea banda la NSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza

Afisa Usalama Mwandamizi wa NSSF,Mfaume Kambangwa akitoa elimu kwa wanachama wa NSSF waliotembelea banda la NSSF namna Mfuko unavyopinga vitendo vya rushwa na kuwa huduma zote zinatolewa bure. Elimu hiyo ya kupinga rushwa katika maeneo ya kazi inatolewa katika Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo wilaya ya Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mradi huo unafika katika Jiji la Dar es Salaam ili kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwenye Mkoa huo.

Wazii mkuu amesema jana alipokea maagizo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa anazungumza kwenye Kongamano la Kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia ambapo aligusa upatikanaji wa majilakini pia akaja kuzungumza upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa na kuagiza kutaka maelezo ya kina kuhusu changamoto hiyo.

"Sasa hivi tuna tatizo la upatikanaji wa maji kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo Mikoa hiyo inategemea chanzo Kikuu cha mto Ruvu lakini pia kwa Kigamboni tunategemea visima hivi hivyo kutokana na changamoto hizi naagiza DAWASA kuhakikisha wanafanya kazi kwa masala 24 ili kuhakikisha maji yanaanza kupatikana kwa kutumia chanzo cha Kigamboni" alisema Majaliwa

Amesema Jiji la Dar es Salaam lina mahitaji ya maji Lita Milioni 540 lakini kama tunakuwa na mvua za kutosha basi kutakuwa na uwezekano wa kupata maji Lita Milioni 520 tukiwa na upungufu wa Lita Milioni 20 lakini kwa sasa Jiji la Dar es Salaam linapata Lita Milioni 300 ikiwa na upungufu wa Lita Milioni 220.

Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha maeneo yote yanapata huduma za maji na kazi ya uchimbaji visima pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya maji inaendelea ili kufikia matamanio ya Mheshimiwa Rais Samia ya kufikisha huduma ya maji karibu na makazi ya wananchi.

Akizungumza baada ya kukagua na kuwasha pampu ya maji katika mradi wa Visima vya Maji kwenye mradi wa Kisarawe II uliopo Kigamboni, Waziri Mkuu amesema visima hivyo ambavyo vinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 70 kwa siku vitasaidia katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam.

“Katika kipindi hiki ambacho kiwango cha maji katika Mto Ruvu kimepungua uzalishaji wa maji nao umepungua na kufikia lita milioni 300 kwa siku, hivyo kusababisha upungufu wa lita milioni 244. Kwa sasa tukiingiza lita milioni 70 kutoka katika mradi huu wa visima vya Kigamboni tutakuwa na upungufu wa lita milioni 174, hivyo tutaupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika baadi ya maeneo.”

Waziri Mkuu amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Mheshimiwa Rais Samia alitoa shilingi bilioni 25 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uchimbaji visima 10 katika eneo la Kigamboni, ambapo kati yake visima saba ndio vimewezesha upatikanaji wa lita milioni 70. Amewaagiza watendaji DAWASA waendelee na uchimbaji wa visima vingine.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akishika maji mara baada ya kuzindua maji kwa ajili ya wakazi wa Kigamboni na Dar es Salaam alipotembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akifungua koki ya maji kuashiria uzimduzi wa maji wa Kisarawe II kwa ajili ya wakazi wa Dar es Salaamwakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza kuhusu namna wanavyoendelea na jitihada za kupunguza ukali wa mgao kwa kuhakikisha wanapeleka maji Dar es Salaam kwa kutumia mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ya kukagua maendeleo ya mradi huo Pamoja na kuzindua maji yatakayotumika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza kuhusu kupokea maagizo aliyopewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alipokagua maendeleo ya mradi wa maji wa kukagua ujenzi wa Tanki, uchimbaji wa visima kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II katika wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa moja ya visima vinavyozalisha maji kwenye mradi wa Kisarawe II wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kutoka kwenye mradi huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA lililopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II hii ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza jambo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA lililopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi pamoja na waandishi wa habari wakati wa kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso pamoja, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakiendelea na ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kutoka kwenye mradi huo.