Na Ivon Samson-MAELEZO 

Hayawi hayawi sasa yamekuwa ni siku 66 pekee zimebaki mashindano ya AFCON kuanza ifikapo April 14, 2019, ambapo pazia la michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 litafunguliwa. 

Mkurugenzi wa Baraza la Michezo la Taifa-BMT,Yusuph Dingo, amesema kuwa mpaka sasa maandalizi yanaenda vizuri na yamekamilika kwa asilimia kubwa.ikiwemo miundombinu ya viwanja, usafiri, na hoteli ambazo wageni watafikia. 

Dingo, amesema “Michuano hiyo ambayo itakayofanyika Jijini Dar-es-salaam, itajumuisha timu nane katika makundi mawili, ambapo kundi A kuna wenyeji Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda. Aidha, kundi B litajumuisha mataifa ya Guinea, Cameroon,Morocco na Senegal.Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa michuano hii na imewekeka historia mpya kwa nchi za Afrika Mashariki”. 

Aidha, viwanja vitatu pekee ndiyo vitatumika kwenye michuano hii ambavyo ni uwanja wa Taifa,Uhuru na Azam Complex unaomilikiwa na klabu ya Azam FC.Hakika hii fursa hadhimu kwa wapenda mchezo wa soka hapa nchini Tanzania kushudia mataifa ya kigeni yakija kwenye ardhi yetu ya 

Dingo Alienda mbali zaidi kwa kueleza kwamba hii fursa kubwa zaidi kutokea nchini kwetu hivyo ni vyema tukajipanga vizuri ili wageni wakija waje kuona uzuri, sifa nzuri ya Tanzania na mabalozi wazuri kusimulia mazuri ya nchi yetu. 

"Tumejipanga vyema sana pia tutashirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania-TTB kuhakikisha tunatangaza vivutio vyetu vya utalii vilivyopo kwani hii fursa pekee na ukizingatia watu wengi wanaingia nchini kwetu.Tuna ndege za kisasa hivyo hizo zinakuwa chachu kwa wageni ambao watapenda kwenda mikoa mbalimbali yenye vivutio. 

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Micheza Tanzania-TFF Ammy Ninje, amesema kuwa maandalizi ya timu yetu yanaenda vizuri na wiki mbili zijazo kikosi hicho cha Serengeti Boys kitaenda nchini Uturuki ili kuweka kambi ya kujiandaa na michuano hiyo. 

Aidha, TFF wamepanga kuongeza mwalimu kwenye benchi la ufundi ili aweze kushirikiana na mwalimu Oscer Mirambo na Hemedi Moroco ili kufanya vijana wapate mazoezi zaidi na hatimaye kupata ushindi katika michuano hiyo. 

Timu ya Serengeti Boys inajumuisha wachezaji………ambao wamechaguliwa kutokana na vijana walioshiriki michezo mbalimbali ya Kopa Cocacola, Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania .-UMISETA 

08 Februari 2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...