Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KUNDI la vichekesho la Mizengwe linaloundwa na watu limewavunja watu mbavu kutokana na vichekesho vyao walivyokuwa wanavitoa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wasanii hao wa vichekesho ambao wapo watano leo baada ya kupanda jukwaani walisema kuwa wamefika wanne kwani mwenzao mmoja amekwenda nchini India kwa ajili ya mazungumzo na Amitha Bachan.

Kitendo cha kueleza mwenzao yupo nchini India na anamazungumzo na Amitha Bachan watu waliokuwa ukumbini waliangua kucheka kwa sauti kubwa.

"Kundi la Mizengwe linaundwa na watu watano,ila leo mwenzetu mmoja anayefahamika kwa jina la Mzee Matata amekwenda India kuzungumza na Amitha Bachan.Hivyo tupo sisi tu," amesema  mmoja wa wasanii hao...watu kicheko.

Hata hivyo Mchekeshaji wa kundi hilo Rashid Coster a.k.a Mkongoman aliamua kutoa vichekesho vya aina yake na aliwavunja mbavu watu baada ya kusema kwao muhimu ni kuvaa kwani kula nani anakuona.

"Kwetu sisi Wasanii kula sio jambo muhimu sana kwani tumbo halina kioo lakini kuvaa ndio muhimu sana kwani nguo ndio zinaonekana," amesema Mkongaman.

Kwa upande wake Mwanadada pekee katika kundi hilo la Mizengwe Jesca alitumia nafasi hiyo kwa kutumia sanaa yake ya uigizaji kuzungumzia athari za dawa za kulevya.

Amesema wanaotumia dawa za kulevya hata ndoto za maisha yao zinatoweka na hivyo kuwaomba Watanzania na hasa wa wasanii kwa ujumla kuacha kutumia dawa za kulevya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...