Kururunfa kata, huko Okinawa,Japan.
Shihan Magoma na sensei Rumadha Fundi 1980 Zanaki Dojo, maadhimisho ya miaka 7 ya Goju Ryu Jundokan Tanzania.
Shishochin kata, Okinawa, Japan
Baada ya kumaliza kongamano la maadhimisho ya miaka 65 ya
chama cha Goju Ryu Karate -Do Jundokan mwezi wa November mwaka 2018 huko
Tomigusuku, Okinawa, Japan, sensei Rumadha Fundi na wenzie washiriki toka nchi
zaidi ya 25 walitembelea makumbusho ya sanaa ya Karate iliyomo ndani ya ukumbi
maalum kwa shughuli za karate. Ukumbi huo maarufu wa " Okinawa
Karate Kaikan" ulifunguliwa miaka michache na mfalme Akihito wa japan
kwa lengo la kuwa na maadhimisho ya michezo ya Karate visiwani humo.
Mambo mengi muhimu katika ziara hiyo ilikuwa pia kuona
vitabu na video mbalimbali za waasisi wa mchezo wa karate kabla hata karate
kuwa imebuniwa mnamo karne ya 18,ikiwa ni mafunzo ya siri na ikiwa imegawanywa
katika vitongoji vitatu vya visiwani hapo. Utamaduni huo wa Okinawa wa sanaa
hii wakati huo ilikuwa unaitwa "
Te", ikimaanisha mkono. Hivyo ndivyo kila kitongoji kimoja kati hivyo
vitatu yaani hiyo miji ya Shuri, Tomari na Naha ikajipatia sanaa ya kujilinda
kwa majina ya, Shuri-Te, Tomari-Te,
na Naha-Te
SHURI-TE:
Watu muhimu sana katika mchango wa sanaa ya Karate huko
Okinawa na huenda watu na mashabiki wengi wa Karate hawamfahamu, ni mwalimu
aitwae Matsumura Sokon, alifundisha magwiji wengi waliokuja baadae kuanzisha
mitindo mingi sana ya Karate huko Okinawa.
Baadhi ya walimu maarufu na
niwanafunzi wa Matsumura Sokon ( Alijifunza sanaa ya kujilinda toka kwa
Sakugawa Kanga), ni:Anko Asato, Anko Itosu
(mpaka hii leo anajulikana kama baba wa karate ya kisasa ), moja ya
wanafunzi wa Itosu ni Gichin Funakoshi wa Shotokan, Chotoku Kyan ( Kachangia
sana mtindo wa Shorin Ryu), Choshin
Chibana ( mwanzilishi wa mtindo wa Shorin Ryu), na Gichin Funakoshi(
Mwanzilishi wa mtindo wa Shotokan), ambae
aliendelea na mafunzo chini ya Anko Itosu. Pia vile vile yupo mwengine ambae ni
mwanafunzi wa Matsumura Sokon, anaitwa Kenwa Mabuni na Tatsuo Shimabuku (
Mwanzilishi wa mtindo wa Isshin Ryu).
Mitindo ya sasa ya Karate iliyozaliwa na ushawishi wa
misingi ya Shuri-Te ni: Shotokan,
Wado Ryu, Motobu Ryu, Shorin Ryu, Shudokan, na Shorinji Ryu ( Mtindo uliobuniwa
na Sakugawa Kanga, mwalimu wa Matsumura Sokon).
TOMARI-TE:
Chanzo cha sanaa hii ni kitongoji cha Tomari ambayo ni
bandari kuu kisiwani hapo tokea mnamo karne ya 17. Walimu muhimi toka hapo
walikuwa ni:
Kosaku Matsumura, Motobu Choki (Mwanzilishi wa Motobu
Ryu), Yamazato Gikei, Kyan Chotoku ni baadhi ya walimu waliokuwa wanajifunza
sanaa za vitongoji zaidi ya kimoja.
Mitindo iliyozaliwa chini ya ushawishi wa Tomari-Te ni: Motobu Ryu, Shorinji Ryu,
Matsubayashi Ryu, na Gohaku kai. Hapo mitindo iliyorudiwa mara mbili
inamaanisha waasisi hao walijifunza pande zote mbili za miji hito ya Okinawa.
NAHA-TE.
Kabla ya vita kuu ya pili ya duania, mji wa Naha ulikuwa
ndio mjimmaarufu wa biashara katika visiwa vya Ryu Kyu. Hivyo ndivyo uliwavutia
wafanya biashara wengi toka China . Hivyo ndivyo sanaa ya Naha-Te ilikuwa na
ushawishi mwingi wa mbinu toka kusini mwa China hasa kwa mbinu za "Fujian White Cranes Systems".
Kulikuwa na msongamano mkubwa wa wahamiaji wa kibiashara wa China katika mji wa
Naha. Mtu ambaye alikwenda China kujifunza mbinu hizo za kichina na baadae
kurudi Okinawa , alikuwa mwalimu Karyo Higaonna ambaye ndio kiini kikubwa cha
kuiunganisha sanaa ya Kichina na Naha-Te mnamo moaka ya 1880.
Baadhi ya walimu wachache maarufu toka mji wa Naha ni:
Karyo Higaonna (Mwalimu wa Chojun Miyagi), Chojun Miyagi
(Mwanzilishi wa mtindo wa Goju Ryu) ambaye pia alikwenda China ya kusini
kujifunza sanaa za Kichina, Kyoda Juhatsu, Kenwa Mabuni (Mwanzilishi wa mtindo
wa Shito Ryu), na Uechi Kanbun (Mwanzilishi wa mtindo wa Uechi Ryu).
Mitindo ya karate
iliyozaliwa chini ya ushawishi wa Naha-Te
ni:
Okinawa Goju Ryu, Uechi Ryu na Shito Ryu.
Pia vilevile kwa manufaa ya kuwaelimisha wanakarate wa
cha na historia za Kata mitindo tofauti, napenda vilevile kusitaja kata hizo na
kimbuko lake kila moja.
Kata
za Shuri-Te ni : Naihanchi,
Pinan, Kusanku, Passai, Jion, Jitte, Rohai, Chinto na Gojushisho.
Kata
za Tomari-Te ni:Naihanchi, Rohai, Passai, Wankan, Wansu na
Sesan.
Kata
za Naha -Te ni : Sanchin,
Saifa, Seiyunchin, Shisochin, Seipai, Seisa, Tensho, Kururunfa, na Suparinpei.
Nakala hii imenukuliwa na Sensei Rumadha Fundi toka
makumbusho ya Karate katika "Okinawa Karate Kaikan”, huko Tomigusuku,
Okinawa, Japan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...