Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli amesema kuwa amefurahishwa mno  na ushindi wa mabao 3-0 ambao timu ya Tanzania ' Taifa Stars'  imeshinda dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda na kufuzu kucheza fainali za AFCON nchini Misri Baadaye mwaka huu.

Akizungumza kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mpira kumalizika Rais amesema ushindi wa Taifa Stars ni heshima kwa Tanzania na kwamba leo ameona mpira mkubwa kulinganisha na siku za nyuma.

Hata hivyo Rais Magufuli amezungumzia mchezo huo na kubwa zaidi ametoa pongezi kwa wachezaji kwa mpira ambao wameuonesha na hakika amefurahi sana kwani mpira aliokuwa akitamani kuuona leo ameuona.

"Ni heshima kubwa kwa nchi yetu,hongereni wachezaji,hongereni wote ambao mmefanikisha ushindi .Kwanu nimefurahi sana na leo nilisema sitaenda uwanjani ili niuone hapa hapa Ikulu.

"Ni heshima kubwa kwa nchi yetu," amesema Rais Magufuli huku akieleza matokeo ya Lesotho na Cape Verde nayo yamemfurahisha kwani yameivusha Tanzania kwenda Misri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...