Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaamuru wadhamini wa Zitto Kabwe pamoja na yeye mwenyewe kufika mahakamani hapo Aprili 9, 2019 na kujieleza kwa nini mshtakiwa Zitto leo hajafika mahakamani.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakamani hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Mapema, Wakili wa serikali Wankyo Simon alidai kuwa kesi dhidi ya Zitto leo Machi 11, 2019 imekuja kwa ajili ya kutajwa, na wana dhahidi mmoja ambaye yuko tayari kutoa ushahidi wake lakini mshtakiwa Zitto hayupo.

Hata hivyo, Wakili anayemtetea Zitto, Steven Mwakibolwa amedai kuwa amepata taarifa kutoka kwa ndugu yake Zitto, Vincent Kasafa kuwa Zitto ni mgonjwa, ambapo alipotakiwa na mahakama kueleza, mtoa taarifa hiyo, amedai kuwa yeye ni shemeji yake na Zitto, mke wake Zitto alimpigia simu na kumtaarifu kuwa Zitto anaumwa lakini yeye hajui yuko wapi.

Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Shahidi amemwambia, "umepewa taarifa huna hakika, tusitafutane maneno, wadhamini siku ya kesi wafike mahakamani na waeleze kwa nini leo hawajafika", pia hakimu Shaidi amemuonya Shahidi ASP Shamira Nkoma kufika Aprili 9,2019 mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Zitto ambaye yupo nje kwa dhamana, katika kesi hiyo, anadaiwa Oktoba 28, mwaka jana, Zitto akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT_Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...