NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

WIMBI la mamba katika ukanda wa mto Ruvu, kata ya Kilangalanga, Kibaha Vijijini mkoani Pwani linadaiwa kuwa wengi hali inayojenga hofu kwa wananchi ambapo hadi sasa watu wawili wameshajeruhiwa na mamba hao. 

Aidha  wanyama waitwao Kiboko wanadaiwa kuvamia baadhi ya mashamba ya watu na kuharibu mazao ikiwemo mpunga. 

Akielezea tukio hilo, diwani wa kata ya Kilangalanga, Mwajuma Denge aliomba idara husika isikie kilio chao kwa kuvuna mamba badala ya kuwatega. 

"Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana mmama mmoja alijeruhiwa mkono na mamba na alifikishwa Tumbi hospital ambako anatakiwa kiasi cha sh. 500,000 hadi sasa ili aweze kufanyiwa operesheni na matibabu zaidi "

"Wiki mbili zilizopita pia mama mwingine amejeruhiwa makalio na alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi na alitibiwa kisha amehamishiwa hospital ya Tumbi anaendelea na matibabu hadi sasa. "alielezea Mwajuma. 

Mwajuma alisema kuwa, viboko nao ni kero nyingine wanaomba idara ya wanyamapori waende wakaangalie namna ya kuwadhibiti kwani hawajui wanapotokea. 

"Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa alichukua hatua na kufanya juhudi binafsi kupeleka watu wa maliasili ambao wanaendelea na jitihada zaidi." 

"Kutokana na mto kujaa na kuweka maji ya rangi ya tope wameshindwa kuwapata mamba hao, na wameacha zoezi hilo, watarudi baada ya wiki moja. "alielezea. 

Nae,  makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,ambae pia ni diwani wa Kikongo Fatma Ngozi alisema tatizo hilo, lipo na kata zilizopita mto huo ikiwa ni sanjali na Dutumi, Mtongani, Kwala,na Kikongo .

Alifafanua, mamba waliwahi kuvunwa tangu miaka ya 90 hivyo wamejaa inabidi wapunguzwe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...