*Hutoa asilimia 80 ya mshahara wake kusaidia wanafunzi, Rais Kenyatta ampongeza

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWALIMU  wa hesabu na fizikia  Peter Makaya Tabichi kutoka eneo la Nakuru  nchini Kenya ameshinda tuzo ya mwalimu bora duniani kwa 2019 na kuibuka na kitita cha dola milioni moja.

Tabichi anafundisha katika shule ya sekondari mchanganyiko ya Keriko Pwani vijijini.

Imeelezwa kuwa Tabichi (36)hutoa asilimia 80 ya mshahara wake wa mwezi kwa watu wasiojiweza na  tuzo hiyo imetolewa katika sherehe iliyofanyika Jumamosi huko  Dubai.

Aidha mwalimu huyo  husaidia wanafunzi wake wasiojiweza  kununua sare za shule na vitabu, akizungumza na vyombo vya habari Tabichi amesema;
"Kila siku Afrika tunafungua ukurasa mpya wa maisha. Tuzo hii hainitambui mimi bali inawatambua vijana wa bara hili. Nipo hapa kwa sababu ya kile ambacho wanafunzi wangu wamefanikiwa katika maisha yao,"ameeleza.

Aidha amesema kuwa tuzo hiyo inawapa wanafunzi hao na  imeutangazia  ulimwengu kuwa wanaweza kufanya kitu chochote katika sekta hiyo.

Tabichi aliwabwaga  walimu wengine tisa kutoka sehemu mbalimbali  funiani waliofanikiwa kufika fainali katika kuwania tuzo hiyo ya mwalimu bora huku idadi wa washiriki ikiwa ni 10,000.

Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyata amempongeza mwalimu na kusema kuwa historia yake ni kubwa Afrika na jambo hilo ni kubwa kwao kama taifa na kwake pia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...