NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amesema Serikali inapitia mikataba na makubaliano ya wawekezaji waliopewa kuendesha Hoteli za Kitalii zinazomilikiwa na Serikali kwenye maeneo ya Hifadhi. 

Kanyasu alitoa kauli baada ya kutembelea Hoteli ya Ngorongoro Wild Life Lodge iliyomo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni ziara yake iliyoanzia Hifadhi ya Serengeti, Manyara na kwingineko. 

Naibu Waziri Kanyasu mara baada ya kuzungumza na Mejinementi ya NCAA, alisema kwamba hoteli hizo zilibinafsishwa kwa malengo ikiwamo kuona zinaendeshwa kwa faida, kuajiri Watanzania na kulipa kodi. 

“Nitapita kwenye hoteli hizi moja baada ya nyingine kuangalia makubaliano ya kuziendesha ni yale yale au wamekiuka kama wamekiuka basi serikali itaangalia kwanza ushauri lakini kuvunja mkataba,” alisema Naibu Waziri Kanyasu. 

Kaimu Mhifadhi wa NCAA Needpeace Wambuya kwa upande wake alisema moja ya jukumu lao n kuhakikisha ukaguzi wa utoaji huduma zenye viwango vya kimataifa unafanywa ndani ya hoteli zilizopo NCAA.

“Kwenye eneo hili la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tuna hoteli kubwa tano ukijumlisha na nyingine za kawaida zinafikia hoteli 11,” alisema Wambuya. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...