Naibu Waziri wa afya na Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine, Ndugulile, amesema anajivunia kuongoza eneo ambalo ardhi yake asilimia 67 imepimwa, jambo ambalo limesaidia kutatua migogoro ya ardhi na kuwa na ardhi inayotambulika.

Naibu waziri huyo wa afya ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akigawa mkataba wa ununuzi wa viwanja kwa wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi nchini.

Ndugulile, amesema kitendo cha KC kupeleka mradi huo ni katika kuendeleza juhudi hizo za Serikali na kuahidi hadi kufika mwaka 2020 wana imani ardhi yote itakuwa imepimwa kwa eneo lilibaki ni asilimia chache.

“Eneo la kisarawe2 ni la kimkakati kwa ajili ya biashara na tayari eka 1,000 zimetengwa kwa ajili ya viwanda, hivyo mlioamua kununua viwanja hapa hamtajuta kwani huko mbele ya Kigamboni inatarajiwa kuwa kitovu cha biashara katika mkoa wa Dar es Salaam ,”amesema Ndugulile.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi, amesema viwanja hivyo huuzwa kwa mkopo ambapo mteja akishalipa asilimia 20 ya bei ya kiwanja husika, inayobaki analipa kwa miaka miwili.

Mwinyi amebainisha kuwa wamekuja na mkakati huo kama njia ya kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini kumiliki ardhi ambapo ekari 200 zilizopimwa zimechukuliwa na wananchi zaidi ya 900.

“Moja ya changamoto tuliyoipata katika kupata wateja ni pamoja na suala la wananchi kuamini kama kweli watapata viwanja kwa kile walichodai wameshatapeliwa sana huko nyuma, hivyo tunajitahidi kuwaonyesha sisi hatupo hivyo kwa kuweka kila kitu wazi, hivyo tunaomba wananchi watuamini tumekuja kuleta suluhisho la migogoro ya ardhi,” amesema.

Naye Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuna alichojifunza kuhusu umuhimu wa kuwa na maeneo ya kupimwa kutoka Kigamboni, ustaarabu ambao amesema atapeleka elimu hiyo Ilala ili nao waige mfano huo mzuri.

Wananchi waliokabidhiwa mikataba akiwemo Eleotheria Namikowi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala na Bashiru Mkabala wa Ubungo, wamesema moja ya jambo lililowashawishi kuchukua viwanja hivyo ni pamoja na kukopeshwa vifaa vya ujenzi.
Mbunge wa Kigamboni ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi, ambapo ameiomba kampuni ya KC isiwe chanzo cha migogoro ya ardhi katika hafla ya kugawa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwa wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi jijini Dar es Salaam.
Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi ambapo ameipongeza kampuni ya KC kwa kuwakopesha wananchi viwanja bila riba katika hafla ya kugawa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwananchi wa Mtaa wa Mwasonga, kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi akisoma hotuba katika hafla kugawa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwananchi wa mtaa wa Mwasonga, kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile (katikati) akizindua utoaji wa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi jijini Dar es Salaam. Kushoto Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.(kulia) Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi.
Mbunge wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akisalimina na wananchi wa Kigamboni.( Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Maafisa wa kampuni ya KC wakiwagawia mikataba ya ununuzi wa viwanja wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, kata ya Kisarawe2, wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...