Na Karama Kenyunko, globu ya jamii 

WATU saba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la tuhuma za wizi wa mapipa 20 ya mabaki ya madini yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 900. 

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Mbando, Wakili wa Serikali Jenifa Masue amewataja washtakiwa hao ni Jacob Kihombo, Yahaya Masoud, Mbaraka Lipinda, Ramadhani Zombe, Waziri Kibua, Mustapha Mnyika na Richard Sàngana. 

Imedaiwa kati Februari 6 na 7 mwaka huu ndani ni Jiji la Dar es Salaam washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa la kula njama ya wizi wa mali inayosafilishwa. 

Katika shitaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa waliiba mali hiyo ambayo ni mapipa 20 ya mabaki ya madini aina ya Tantalite Concentrates yenye thamani ya Sh.938,339,907 mali ya Kampuni ya Bollore Transport and Logistics. 

Shitaka la tatu linalomkabili mshtakiwa Zombe peke yake ambaye ni mlinzi, anadaiwa siku hiyo akiwa mwajiriwa wa Kampuni ya Bollore, kama mlinzi, alishindwa kuzuia kutendeka kwa kosa la wizi wa mapipa hayo ya madini. 

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka katika taasisi zinazotambulika na serikali watakaosaini bondi ya Sh. milioni 52 kila mmoja. 

Pia mdhamini au mshitakiwa ametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya milioni 52. Kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...