Na Karama Kenyunko, globu ya janii.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa muda wa mwezi mmoja Kamishna wa Idara ya Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala, kuhakikishia kuwa anamkabidhi orodha ya mapapa wa biashara ya kuingiza na kusafirisha wahamiaji haramu nchini.

Waziri Lugola ametoa maagizo hayo leo Aprili 4, 2019 jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa ngazi ya juu uliohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi juu ya tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).

Mkutano huo wa siku mbili unalengo la kutafuta mwarobaini wa tatizo la wahamiaji.Lugola amesema, wahamiaji haramu wasingeweza kufanikiwa kuingia nchini kwa njia yoyote kama miongoni mwa watanzania hawatawasaidia, hivyo amewaasa waache kabisa kiwapokea na kuwasaidia kwa namna yoyote ile iwe kwa kuwapa chakula kuwasafirisha au kuwahifadhi katika jengo lolote ambapo hilo likifanyika, tatizo lotakwisha.

Aidha amemtaka, kamishna Generali, sasa akae na timu yake ili walifanyie kazi hili tatizo ili ndani ya mwezi mmoja aje na orodha ya madalali wanaosaidia wahamiaji haramu hata kama wako nje ya nchi wanasakwa na kukamatwa ili kuvunja mtandao.

"Tunataka hao madalali wenyewe kabisa wasakwe na wakamatwe maana tunaishia kukamata dereva wa fuso ambae amewapakia hao wahamiaji na tunawaacha wahusika wenyewe wakitembea angalau basi kwa uchache uje na orodha ya hawa madalali, wawili watatu hata kama tunaambiwa wako nchi nyinginie za jirani na ni wenzetu tuweze kutumia sheria tulizonazo za kuwakamata na kuwaleta tuhakikishe kwamba mtandao huu tunaumaliza" amesema Lugola

Aidha amesema katika kupamba na tatizo la wahamiaji Haramu wamependekeza kuwa, wahamiaji haramu sasa wasiwe wanapelekwa mahakamani na kufungwa magerezani, badala yake wakikamatwa kuwe na njia mbadala, ya kuwarudisha kwao baada siku chache. Ambapo shirika la kimataifa la Uhamiaji limeahidi kuwa linatoa garama za kuwaaafirisha.

Kwa upande wake, Kamishna Generali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, amesema, mkutano huo unalengo la kusaka suluhu juu ya changamoto hiyo ya wahamiaji haramu kwenye nchi hizo tatu kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.

Amesema, changamoto ni kubwa na inahitajika kupata suluhu ya kudumu, ndiyo maana tumekutana hapa kwa kushirikiana na wenzetu wa wa nchi hizi tatu ili tuweze kupata ufumbuzi wa kudumu jambo ambalo tunaamini kuwa tutafanikiwa," amesema Dk. Makakala.

Naye, Balozi wa Wizara ya mambo ya Nje Kenya, Michael Oyugi amesema, nchi yake imeongeza idadi ya maafisa usalama wa Uhamiaji mipakani Ili wahamiaji haramu wanaoingia Kenya na kukimbia nchi zingine wanamalizika kabisa. 

Amesema, Mipaka kati ya nchi ya Kenya name Ethiopia ni mirefu sana, ni kama mita 700 hivyo siyo rahisi kuweka maafisa usalama wa Uhamiaji katika mipaka hiyo yote hivyo Wengi wa hawa wahamiaji haramu hupita njia zisizohalali 'njia za panya' ambazo hazina maafisa wa Uhamiaji hivyo ni ngumu sana kuwakamata. 

Amesema, makubaliano hayo yote yatasaidia sana kupunguza wahamiaji haramu, lakini inatupasa kwenda taratibu kwani jambo hili ni ngumu na hatuwezi kulisuluhisha Mara moja.

"Tumeishakuwa na mikutano Kadhaa, ambayo inashughulikia namna ya kutatua tatizo hili pole pole na sasa tunatafuta njia ya kumaliza tatizo hili na haya makibaliano ambayo tunatoka nayo hapa tunayachukua na kwenda kuyafanyia kazi.
Waziri wa Mbamo ya Ndani nchini,Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa ambapo alimuagiza Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anakuwa na orodha ya majina ya madalali wanouhusika kuwaingiza wahamiaji haramu nchini (Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala (kulia) akizungumz na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,mara baada ya kufunguliwa mkutano wa ngazi ya juu uliohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi kuhusu tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala (wapili kushoto) akiwa pamoja na vingonzi wa nchi mbalimbali wakisani hati za makubaliano ya uliohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi kuhusu tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katikati akibadilisha hati zilizohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi kuhusu kukomesha tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...