NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani imewafikisha mahakamani mwenyekiti wa Kitongoji cha Razaba ,namba 4 ,Makurunge Bagamoyo Siasa Kasanura, na wenzake wanne kwa kosa la kutoa hongo ya sh.270,000 kwa askari polisi kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha 
Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007. 

Washitakiwa hao,wakiwemo wafanyabiashara wawili Idrisa Machano na Ndaju Kivalia, pamoja na mlinzi wa kampuni ya Bagamoyo Sugar Shabani Funga kwa kosa la kutoa rushwa hiyo machi, 2019 kwa askari polisi wa ofisi ya mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Pwani ili wasiwakamate wakati wakiendelea kufanya biashara haramu ya mkaa na magendo katika kitongoji hicho.

Kamanda wa TAKUKURU Pwani, Susan Raymond alieleza, askari hao walikuwa kwenye operesheni maalumu ya kudhibiti uhalifu katika kitongoji cha Razaba . 

Alisema, kitendo cha askari hao kudhibiti mianya ya biashara haramu ya mkaa na magendo kilipelekea wafanyabiashara haramu, wakiongozwa na mwenyekiti wao Siasa Kasanura kwenda kuwashawishi polisi kwa kuwapa hongo kwa ili wasiwakamate na wawaruhusu waendelee na biashara hiyo haramu. 

Susan alibainisha, washtakiwa hao wamefunguliwa mashitaka ya ya jinai namba 146 ya mwaka 2019 katika Mahakama ya wilaya Bagamoyo kwa kosa la kutoa hongo hiyo, kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba. 11/2007. 

"Washtakiwa wote wanne wakisomewa mashtaka na mwanasheria wa TAKUKURU, Beatrice Ngogo mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Tumaini wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo, walikiri kutende kosa"

"Na ikumbukwe kwamba mtoaji na mtoa rushwa wote ni kosa"alisisitiza Suzan. 

Kamanda huyo alifafanua, kutokana na kukiri kutenda kosa hilo mahakama imewatia hatiani na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila mmoja ama kulipa faini ambapo watuhumiwa wameamua kulipa faini na wamewekwa mahabusu wakisubiri kukamilisha malipo 
hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...