Na Woinde Shizza, Michuzi TV Arusha

Mkuu Wa Wilaya  Arumeru Jerry Muro amewakikishia wananchi wake ataendelea kutatua  changamoto zinazo wakabili ikiwemo changamoto za ardhi.

Ameyasema hayo Leo wakati akimtambulisha  kamanda Wa polisi mpya Wa mkoa Wa Arusha Jonathan Shana  alipofanya ziara ya kutembelea halmashauri hiyo.

Alisema kuwa ofisi yake imeweka mkakati Wa kutatua kero za wananchi wake ambapo ofisi yake imeweka wanasheria wanne  ambao watawasaidia wananchi wasio  kuwa na uwezo .

"Kuna wananchi wengi ambao wana kesi mbalimbali na wanataka msaada Wa kisheria lakini wanashidwa kuweka wanasheria kutokuwa na uwezo hivyo nimeamua kuwatafutia wanasheria hawa wanne ambao nitawalipa Mimi mwenyewe kwa mshahara wangu Mdogo ninaopewa ili wafanye Kazi yakutatua matatizo ya wananchi yanaohusu sheria " alisema Muro.

Akiongea na wananchi kamanda Wa polisi mkoa Wa Arusha Jonathan Shana aliwakikishia wananchi Wa Wilaya ya Meru  kuondoa askari yeyote atakiuka taratibu na kanuni za Kazi yao kwa kuchafua sifa za jeshi la polisi.

"Napenda kuwaahaidi wananchi kuwa sitamfumbia macho askari yeyote ambae atakiuka sheria ,na Mwananchi yeyote ambae utaona askari yeyote anaekiuka sheria  chukua simu nipigie simu nimshughulikie na naahidi nitasimamia vyema na sitamvumbia maji" alisema kamanda

Wakati huo huo mkurugenzi Wa halmashaiuri ya Meru  Mhe. Emanuel Mkongo alimuhakikishia kamanda Wa polisi Wa mkoa Wa Arusha ulinzi na Amani katika kipindi cha uchaguzi Wa ubunge Wa jimbo la Arumeru mashariki  unaotarajiwa kufanyika mapema mei 19.

Alisema kuwa  mpaka sasa jumla ya wagombea wa vyama 11  wamechukuwa fomu za kugombea na leo april 19 ndio mwisho Wa kurudisha fomu.  

"Vyama hivyo vilivyochukuwa fomu NCCR mageuzi,CUF,ADA TADEA,Chama cha mapinduzi (CCM),AAFP,SAU,Demokrasia makini,DP pamoja na UPDP vyama vyote hivi vimesimamisha wagombea na wanatarajia kurudisha  fomu Kesho" alisema Mkongo.
Uchaguzi huu unafanyika Mara baada ya mbunge Wa jimbo hilo kuvuliwa ubunge Joshua Nasari kutona na kutouzuria vikao vitatu vya Bunge bila kutona taarifa yoyote kwa spika Wa Bunge. 

Kamanda Wa polisi mkoa Wa Arusha Afande Jonathan Shana akiongea na wananchi nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru  Nhe. Jerry Muro wa kwanza kulia 

 Mkurugenzi Wa halmashauri ya Meru Mhe. Emmanuel Mkongoa kiongea  na waandishi wa habari ofisini kwake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...