Je, unatumiaje fani yako? Kama Daktari Pechier?  manufaa yanayoletwa na ujuzi wako  katika jamii ni yapi? hasi au chanya?

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
DAKTARI mmoja nchini Ufaransa Frederic Pechier (47) ameshtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kuwapa sumu zaidi ya wagonjwa 17 ikiwa bado yupo katika  uchunguzi wa vifo vya watu 9 alivyosababisha kwa wagonjwa wakati akifanya upasuaji.

Kwa mujibu wa jarida la DailyMail imeelezwa kuwa daktari huyo amekuwa na tabia ya kuwapa sumu wagonjwa hao kwa malengo ya kuonesha ujuzi wake wa namna anavyoweza kuokoa maisha ya wagonjwa hao.

Daktari huyo anayefanya kazi katika hospitali moja huko Mashariki mwa Mji wa Besancon anashukiwa kwa kuwapa sumu wagonjwa hao wakati akiwafanyia upasuaji kwa kuwapa dawa zilizoathiri mfumo wa moyo na baadaye kujaribu kuwatibu ili kuokoa maisha yao.

Pechier amehusishwa na matukio 24 kati ya 66 na bado yupo chini ya ulinzi licha ya kukana madai hayo ambayo tayari ushahidi umetolewa kwa vifo 9 vilivyotokea na matukio 24 kati 66 yamethibitishwa kutokea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...