Mmoja wa viongozi kutoka mashirika yaliyoungana kuzungumzia masuala yanayohusu maliasili nchini Tanzania akitoa shukrani kwa waandishi wa habari kwa kushiriki mafunzo ya kuwajengewa uwezo kwani anaamini umafunzo hayo yatakuwa chachua kaika kuandika habari.

Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) Zakaria Faustine akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uelewa kuhusu masuala yanayohusu maliasili ikiwemo ardhi.Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.

Mtoa mada katika mafunzo hayo Mary Ndaro ambaye pia ni Mratibu wa programu ya Ardhi Yetu (AYP) kutoka Care Tanzania akielezea umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari za ardhi na hasa kwa kuangalia usawa wa kijinsia.
Waandishi wa habari wakiendelea kupata mafunzo kuhusu namna bora ya kuandika habari zinazohusua maliasili nchini kutoka kwa watoa mada.
Wakili Masalu Luhula kutoka Jumuiko la Maliasili Tazanzia  akifafanua masuala mbalimbali ya kisheria katika sekta ya ardhi nchini ambapo pia alitumia mafunzo hayo kueleza namna sheria za ardhi zinavyofanya kazi na umuhimu wake katika kutatua migogoro katika jamii.
Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la The Citezen akitoa maelezo kuhusu uzoefu wake katika kuandika habari zinazohusu ardhi na maliasili nchini.




Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


JUMUIKO la Maliasili Tanzania limeishauri Serikali kujiikita katika kuendelea kutatua migogoro ya ardhi nchini huku wakitoa pongezi zao kwa Serikali kwa namna inavyochukua hatua kwa kuhakikisha migogoro iliyopo inapata ufumbuzi wa kudumu.

Pia Jumuiko hilo limesema kuna kila sababu ya mikataba mibovu ambayo ipo kwenye ardhi kufumuliwa kama ambavyo Rais Dk.John Magufuli alivyofumua mikataba mibovu iliyoingiwa kwenye sekta ya madini huku wakisisitiza wao wako tayari kusaidiana na Serikali katika hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) Zakaria Faustine amesema Jumuiko hilo na mashariki mengine zaidi ya 18 wamekuwa wakishirikiana katika eneo la maliasili na hasa ardhi na wanaona kazi nzuri inayofanywa na Rais na Serikali katika kutafuta utatuzi wa migogoro ya ardhi.

"Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) pamoja na Tanzania Land Alliance (TALA)tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli kwa hatua inazochukua kutataa kero za wananchi wa maeneo mbalimbali.

"Kwetu sisi ni faraja kubwa lakini nitumie nafasi hii kutoa rai kwa Serikali tunafahamu bado kuna migogoro katika sekta ya ardhi na hivyo ni vema hatua zaidi zikafanyika kupata ufumbuzi wake.

"Binafsi natamani kuona Rais wetu anaagiza kuangaliwa upya mikataba ambayo imeingiwa katika ardhi na ile ambayo itaonekana hafai basi ifumuliwe kwa maslahi ya Watanzania wote,"amesema Faustine.

Akifafanua zaidi wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Jumuiko hilo kwa kushirikiana na TALA kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za ardhi, amesema wamefurahishwa pia na hatua ya Serikali kuyarejesha kwa wananchi baadhi ya mashamba makubwa.

Hata hivyo amefafanua pamoja na Serikali kutangaza baadhi ya mashamba makubwa yaliyokuwa yanamilikiwa na watu binafsi wakiwamo wawekezaji, kwa mujibu wa Faustine ni kwamba mashamba hayo bado hajayakabidhiwa kwa wananchi.

"Tunashukuru nia na dhamira njema ya Rais wetu katika kuhakikisha baadhi ya mashamba yanarudishwa kwa wananchi wa maeneo husika baada ya Serikali kutangaza kuyarejesha.Hata hivyo wananchi hawajapewa mashamba hayo kwasababu mlolongo wa kisheria nao ni mrefu na ili mashamba hayo yakabidhiwe kwa wananchi kuna hatua za kisheria ambazo zinapaswa kuchukuliwa.

"Tuko tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha mashamba ambayo yametangazwa kuwa yamerudishwa kwa wananchi kweli yanawafikia ili yatumike kwa shughuli za maendeleo ya Taifa letu,"amesema Faustine.

Amesisitiza Jumuiko la Maliasili Tanzania pamoja na TALA kwa muda mrefu wamekuwa wakishiriki kikamilifu keulimisha jamii kuhusu ardhi na namna nzuri ya kutatua migogo lakini changamoto kubwa hakukuwa na uchukuliwaji hatua wa haraka kama ilivyo sasa.

Kuhusu waandishi wa habari nchini katika kuandika habari zinazohusu ardhi na masuala mengine ya maliasili, Faustine amesema bado kuna changamoto kubwa kwani habari za ardhi hazipewi kipaumbele kama ambavyo inafanyika katika habari nyingine, hivyo wakaona njia sahihi ni kuwaita waandishi wa habari na kisha kuwajengea uwezo.

"Baada ya kuona kuna pengo la waandishi wa habari zinazohusu Maliasili tumeona vema tukaandaa mafunzo alau ya siku mbili ili tuwajengee uwezo. Hivyo tumeamua kutoa mafunzo kwa waandishi zaidi16 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kutoka mikoa tofauti tofauti,"amesema Faustine.

Wakati huo huo waandishi wa habari nchini wamehimizwa kujikita kuandika habari za uchunguzia na hasa zinazohusu maliasili kwa maslahi ya Taifa ambapo Mwandishi mkongwe nchini Deodatus Mfugali alitumia nafasi hiyo kueleza hatua zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuandika habari za uchunguzi.

Akifafanua zaidi wakati akitoa mada iliyohusu namna bora ya kuandika habari za uchunguzi, Mfugale amesema ili waandishi waisaidie nchi yao katika kutatua migogoro ya ardhi wanayo nafasi ya kujikita kuandika habari za uchunguzi."Changamoto kubwa iliyopo waandishi wengi haaandiki habari za uchunguzi kuhusu ardhi na maliasili za nchini.Tumebaki tu kuandika habari za matukio.

"Nitoe rai kwa waandishi wa habari nchini mkiwemo mliopatiwa mafunzo haya jikiteni kuandika habari za uchunguzi kwa kutafuta vyanzo sahihi na kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi yetu badala ya kuangalia maslahi binafsi,"amesisitiza Mfugale.

Waandishi hao wakiwa kwenye mafunzo hayo pia wameelezwa kuwa nchini Tanzania nafasi ya mwanamke kumiliki ardhi bado ni ndogo sana na hivyo inahitajika jitihada za kutoa elimu na hamasa itakayowezesha wanawake kuwa sehemu ya wanaomiliki ardhi.

Mtoa mada katika mafunzo hayo Mary Ndaro ambaye pia ni Mratibu wa programu ya Ardhi Yetu (AYP) kutoka Care Tanzania ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimsha jamii kuwa mwanamke anayo nafasi ya kumiliki kipande cha ardhi.

"Kuna sababu nyingi ambazo zinachangia wanawake wengi kutomiliki ardhi zikiwemo za masuala ya mila, desturi na tamaduni kwani wapo baadhi ya wanawake kutokana na tamaduni zao hata wakipewa ardhi wanakataa kwa madai kuwa ardhi inamilikiwa na wanaume .

"Hii ni changamoto na ni jukumu letu sote kutoa elimu.Tunashukuru kuna maeneo ambayo tumekwenda huko vijijini wanawake wameanza kuona umuhimu wa kuwa na ardhi kwani ndio kila kitu ikiwemo kwa shughuli za kilimo,"amesema Ndaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...