WASICHANA zaidi ya 30 wameungana na sera ya taifa katika kukuza uchumi wao kupitia programu ya mafunzo ya uandaaji na utoaji huduma katika jamii yao ili kujikwamua kiuchumi Programu ya PANDA yenye lengo la kuwawezesha wasichana Kati ya miaka 18-25 kufikia maendeleo kiuchumi, imeanza rasmi katika vipengele vinne (upambaaji, mapishi, uteengenezaji wa kucha na kilimo) pamoja na elimu ya fedha.

Lengo la Programu hii ya Panda ni kuwawezesha wasichana kwa kuwapatia ujuzi na muongozo ili waweze kujiajiri na hapo baadae kuweza kuwaajiri wengine lakini pia kupata muongozo/usimamizi wa kimawazo katika biashara kwa walio watangulia katika vipengele walivyochagua ili waweza kuendesha biashara zao vizuri na kukabiliana na ushindani katika soko.

Kauli mbiu ya Programu hii ni Anza, Kimbia, kaza kwa lengo la kuwapa hamasa wasichana kuanzisha biashara zao na kuwatia moyo katika kuziendeleza biashara hizo vizuri ili kuyafikia malengo waliojiwekea ya kukabiliana na umaskini lakini pia kufikia usawa wa kijinsia.

Programs hii ni ya miezi sita na itaambatana na shughuli mbalimbali; mafunzo kwa vitendo, miezi mitatu ya usimamizi wa kimawazo kwa biashara zao, warsha kwa siku mbili itakaolenga kuwakutanisha wasichana wajasiriamali wachanga pamoja na sekta binafsi kama taasisi za fedha.

Katika utoaji wa mafunzo haya tunashiriaka na DOT, Lavy_product,Mkulima smart,Mama peridot, rachel’s choice na EFM.Tunakaribisha mashirika/watu binafsil ama taasisi yoyote yenye lengo la kumuinua mtoto wa kike( msichana) kiuchumi kuungana nasi katika kuendesha na kuienndeleza programu hii.

HER INITIATIVE ni shirika lisilo la kiserikali na si la kibiashara.Shirika hili limeanzishwa kwa lengo la kuwaelimisha wasichana katika jamii ili waweze kujitambua na kushiriki katika harakati zozote za kijamii zinazohusu au kugusa maisha yao. Dhamira kuu ya shirika ikiwa ni kuwaelimisha na kuwapa wasichana kipaumbele katika jamii ili kuchochea maendeleo ya usawa.
Majaji siku ya usahili ambao pia ni washirika (partners) katika mradi huu wa Panda kutoka Rachel choice event, DOT,mama Peridot na Lavy Product Panda katika kila kipengele cha mradi (Mapambo, Eimu ya fedha, chakula na kucha), wakimsikiliza msichana aliyekua anajielezea katika usaili.
Baadhi ya wasichana waliokuja kwenye usaili, wakijielezea mbele ya majaji.
Mwanzilishi wa Her Initiative akijadiliana masuala mbalimbali na baadhi ya wasichana waliokuja kwenye usaili.
Timu nzima ya Her Initiative pamoja na wasichana waliokuja kwenye usaili wakiwa katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...