Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Morogoro

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu kwenye minada lengo likiwa ni kusogeza karibu huduma kwa wananchi hasa katika kipindi hiki cha usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza katika mnada wa sabasaba uliopo Manispaa ya Morogoro Mkuu wa kitengo cha kushughulikia masuala ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano TCRA Thadayo Ringo amesema kupitia elimu hiyo wananchi wanapata nafasi ya kujua mambo mbali mbali yanayohusu masuala ya mawasiliano.

Aliwataja wadau wengine wanaoshirikiana nao katika kutoa elimu kuwa ni pamoja na makampuni ya simu ambao wamekuwa wakitoa huduma ya kusajili laini kwa kutumia alama za vidole, jeshi la Polisi ambao wamekuwa wakipokea taarifa za uharifu kwa njia ya mtandao na wizi wa simu na makampuni ya visimbusi.

Kwa upandewa wake Afisa usajili wa vitambulisho kutoka Nida mkoani hapa James Malimo alisema kuwa wananchi wengi hawana uelewa kuhusu usajili wa vitambulisho vya Taifa hali ambayo imekuwa ikisababisha malalamiko hasa pale wanapoambiwa kuwa hawajakamilisha nyaraka muhimu za usajili.

Amesema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ambapo wananchi wanadai Nida wamekuwa wakiwasumbua kwa kuwazungusha hata hivyo alifafanua kuwa NIDA haina nia mbaya ya kuwapa usumbufu wananchi bali ni kutaka kupata uhakika wa nyaraka muhimu zinazotakiwa kwenye usajili.

Hata hivyo alisema kuwa wale waliopata namba za vitambulisho vyao wanaweza kupata huduma ya kusajili laini zao za simu kwa kutumia namba hizo wakati wakisubiri vitambulisho.

Naye mkuu wa kitengo cha makosa ya mitandao kutoka jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Inspekta David Kamugisha alisema kuwa yeyote anayepoteza ama kuibiwa simu iliyo na laini lazima afike kwenye kitengo chake ili aweze kutoa taarifa na baadaye apewa nyaraka muhimu itakayomruhusu kurudishiwa laini yake.

Alisema kuwa mbali na kutoa huduma lakini kitengo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa wananchi ya kuepukana na utapeli unaofanya kwa kutumia mitandao na pia kuepukana na makosa yanayofanywa kwa kutumia mitandao hasa mitandao ya kijamii.

Aidha Mkuu wa Kanda ya mashariki mhandisi Lawi Odiero alisema kuwa lengo ni kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu maswala yote yanayohuau Mawasiliano pamoja na muhumu wa usajili wa line za simu kwa kutumia alama za vidole.

Aliwashauri wananchi kuendelea kujiitokeza ili waweze kusajili line zao kwa kutumia alama za vidole na kwamba ni fulsa kwao.
 Wananchi wakiwa katika foleni kwa ajili ya kusajili ili kuweza vitambulisho vya Taifa na kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akitoa akizungumza na waandishi Habari katika Mnada mkoani Morogoro kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
 Mwananchi akitia saini ya kidole kwa ajili ya kupata kitambulusho cha Taifa kinachotolewa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Mnada ulioandaliwa na TCRA  kwa kushirikiana na wadau hao ili kuwa na vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kitengo cha Kushughulikia Masuala ya Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA Thadayo Ringo akizungumza na waandishi wa habari katika Mnada mkoani Morogoro namna wanavyotoa elimu ya Mawasiliano kwa kutumia minada hiyo.
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaoleth Iseko akimpa mteja maelezo namna ya kusajili  laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akihakikisha usajili wake kwa Mtoa huduma wa Kampuni ya Airtel katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.
 Afisa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa NIDA Mkoa wa Morogoro James Malimo akitoa elimu ya usajili wa Vitambulisho katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...