Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MMILIKI wa Blog ya 8020 Fashion, Shamim Omary Mwasha (41) na mume wake, Abdul Nsembo(45) wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa wakikabiliwa na tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.

Akisoma hati ya mashtaka leo Mei 13, 2019  Wakili wa Serikali, Costastine Kakula amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi,Kelvin Mhina kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo Mei 1,2019 wakiwa huko Mbezi beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao walikutwa na gramu 232.70. za Dawa za kulevya kinyume na sheria ya uhujumu uchumi. 
 Hata hivyo,  washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa  kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi  mpaka Mahakama Kuu ama kwa kupata Kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula ameuomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili hatua nyingine iweze kuendelea licha ya kwamba Leo  ndiyo siku ya kwanza kwa kesi hiyo kusomwa Mahakama hapo.

Kesi imeahirishwa hadi Mei 27, 2019 kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Yaani Shamimu ni mpuuzi sana, maujanja yote kumbe muuwaji halafu anapotosha watu kuwa yeye ni mcha Mungu. Yaani hawa mademu wa mjini ni shombo tu ila si wa kuwa nao hata siku moja. Mtu unalilia kuwa tajiri kwa kuua ama kuharibu wenzako? Hawa wasiachiwe mpaka miaka 40 ijayo ili iwe fundisho kwa wenzao kina Kinje na mapapa wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...