Makamu Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Juma Nkamia akiongoza kikao cha Uhamasishaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV) iliyotolewa na wadau kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.  
Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dafrossa Lyimo akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) na Mpango wa Chanjo Kitaifa mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika kikao kilichofanyika leo Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.

Mshauri Mwandamizi wa Mpango wa Kupima saratani ya mlango wa kizazi Kutoka Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji wa elimu ya uzazi (JHPIEGO), Dkt. Mary Giattas akijibu hoja mbali mbali za Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao cha Uhamasishaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV) iliyofanyika katika Ofisi ya Bunge leo Jijini Dodoma.
Mjumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Amina Makilagi akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Uhamasishaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV) iliyotolewa na wadau kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.  Kuanzia kushoto ni Mbunge wa Kilwa kusini, Mhe. Selemani Bungara, Mbunge wa Ludewa, Mhe. Deogratias Ngalawa na Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Said Maulid Mtulia  

Wajumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mshauri Mwandamizi wa Mpango wa Kupima saratani ya mlango wa kizazi Kutoka Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji wa elimu ya uzazi (JHPIEGO), Dkt. Mary Giattas (hayupo kweye picha) wakati wa kikao cha Uhamasishaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV) iliyofanyika katika Ofisi ya Bunge leo Jijini Dodoma. 

 (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...