Mtaalamu wa Afya akimhudumia mmoja wa wasafiri waliokuwa wakipita katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga aliyeigiza kuugua, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019. 
Daktari katika mpaka wa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, Anna Anthony, akiwapima wasafiri wanaopita katika mpaka huo, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019. 
***************************** 

Kufuatia zoezi linaloendelea mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linajikita katika Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019, Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzania na Kenya, katika makundi tofauti wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika 

Kupima kwa vitendo hatua za kujiandaa na kukabili Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa. Wataalam hao wameweza kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza madhara ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa kwa Wanyama na Binadamu. 

Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...