Na Woinde Shizza, Michuzi TV, Arusha
HALMASHAURI ya jiji la Arusha imetiliana saini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 na Kampuni ya Ujenzi ya BQ Constraction limited ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Wadi ya mama na mtoto itakayojengwa kwenye hospital ya wilaya iliyopo eneo la Engutoto. 

Hafla hiyo imetiwa saini leo Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dakta Maulid Madeni, Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro na Mtendaji na mkuu wa kampuni ya BQ, Mhandisi John Bura, kwenye ukumbi wa halmashauri ya jiji la Arusha na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro. 

 Akizungumza mara baada ya utiwaji saini  Kaimu mhandisi wa jiji la Arusha, Samweli Mshuza, amesema jengo hilo ambalo ujenzi wake unatakiwa kuanza leo utachua muda wa miezi saba kukamilika na litakuwa ni la ghorofa moja. 

 Amesema ujenzi wa jengo hilo ni mwendelezo wa ujenzi wa majengo ya hospital hiyo ya wilaya ambapo tayari jengo la wagonjwa wa nje OPD, lenye ghorofa moja limeshakamilika na sasa linatoa huduma ya chanjo. 

 Kwa upande wake mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya BQ ,Mhandisi John Bura, amewahakikishia viongozi wa serikali kuwa ujenzi huo utakamilika ndani ya muda na anatarajia kukabidhi jengo hilo mapema January mwakani. 

 Nae mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqaro, amesema ujenzi wa hospital hiyo utapunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaopata huduma kwenye hospital ya mkoa ya Mount Meru. 

 Amesema upatikanaji wa dawa kwenye hospital za serikali, Vituo vya afya Zanati katika wilaya ya Arusha ni asilimia 98%. 

Mhe. Daqarro amesema majengo mengine yataendelea kujengwa kulingana na upatikanaji wa fedha na tayari huduma zingine zimeshaanza kutolewa kwenye jengo ambalo limeshakamilika . 

Mkuu huyo wa Wilaya pia amesema hatua hiyo ni historia kwani tangia Uhuru wilaya ya Arusha ilikuwa haina hospital ya wilaya na pia kwenye mipango iliyopo ni kujenga kituo cha Afya kata ya Olasti. 

Mkuu wa wilaya ameongeza kuwa muda hautaongezwa hivyo mkandarasi huyo ahakikishe anakamilisha ujenzi ndani ya muda uliowekwa. 

 Kwa upande wake mstahiki Meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro, amesema ujenzi huo unafanywa kwa fedha za ndani na akatoa wito kwa wananchi kuendelea kulipa ushuru na kodi mbalimbali kwa kuwa manufaa yanaonekana. 

 Amesema kuwa atahakikisha jengo hilo linakamilika na hivyo kuweka historia ya kuwa Meya wa awamu ya Tano ambaye Hospital ya wilaya inajengwa
 Mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dkt. Maulid Madeni na  mstahiki Meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro (kulia), wakitia saini ya ujenzi huo.
 Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni akiwa na  mstahiki Meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro. wakikagua eneo la ujenzi huo.
 Picha ya pamoja ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni akiwa na  mstahiki Meya wa jiji la Arusha Karisti Lazaro (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro na wadau na wakandarasi wa mradi  katika eneo la ujenzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...