Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

 Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa nchi za Afrika Mashariki na  Kati (ECASSA)wamejenga kituo cha kimataifa cha kutoa elimu ya hifadhi ya jamii nchini Tanzania ndani ya jiji la Arusha.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chuo hicho Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Jamii Mhe. Antony Mavunde amesema kuwepo kwa chuo hicho katika nchi ya Tanzania ni jambo la muhimu sana kwani swala la utawala bora kwa jamii umekuwa ni hafifu sana katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Amesema kuwa kikwazo na uhafifu ni kutokana na ukosefu wa sheria za kuwa bana watoa huduma na ukosekanaji wa utawala bora kwa jamii umekuwa nikikwazo kikubwa kwa upatikanaji wa huduma za jamii.

Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa chuo hicho, baadhi ya washiriki kutoka nchi za jumuiya hiyo wamesema umuhimu wa elimu ya mifuko ya jamii barani  Afrika itasaidia sana kwani awali walikuwa wanakwenda nje ya Afrika kwa kukosekana kwake na kutumia pesa nyingi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa ECASSA Bw. Oseya Mtaikili kutoka nchini Kenya amesema kuwa kufuata elimu nchi za n’gambo kutafuta elimu kwa hiyo kuwepo kwa chuo hicho hapa Tanzania kitasaidia kupunguza dharama nyingi zinazotumika kwenda kutafuta elimu hiyo

Akizindua kituo hicho Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amesema tatizo la uhaba wa wataalam wa mifuko ya hifadhi za jamii ni kubwa kwa nchi zote za Afrika Mashariki na kwamba uzinduzi wa kituo hicho ni ukombozi mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...