Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Bw. Yefred Myenzi, akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu kilimo cha umwagiliaji. pamoja na mambo mengine kinavyochangia katika pato la Halmashauri hiyo pamoja na kubadilisha Maisha ya wananchi wa Wilaya hiyo.
NA MWANDISHI MAALUM –
SIMANJIRO
IMEELEZWA kuwa kilimo cha
umwagiliaji ni chanzo kikubwa cha
mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwani huingiza shilingi Milioni mia moja ishirini (120) hadi milioni miambili (200) kwa
mwaka na kuinua pato la wananchi wilayani humo.
Hayo yamesemwa leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bwana Yefred Myenzi ambapo amesema serikali ilitoa kiasi cha
takribani shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi na maboresho ya skimu zaa
umwagiliaji sambamba na kuwawezesha wakulima kupata elimu ya kilimo, uendeshaji
na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji
jambo ambalo limepelekea wanachi kujikita zaidi kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuongeza pato la Halmashauri,
“Mazao mengi yanayolimwa katika skimu za umwagiliaji ni
mpunga na mazao menginge ya Mboga mboga,
lakini pia kuna mazao ambayo hayalimwi katika skimu hizo kama vile Matama,
Uwele na Shayiri zao ambalo linatumika kama malighafi katika viwanda vingi vya beer nchini.” Alisema Bw. Myenzi
Bw. Myenzi alisema kuwa Skimu hizo zimesaidia kuwepo na
chakula cha kutosha na Usalama wa chakula katika Wilaya hiyo, Pamoja na kwamba
Kilimo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa na pamoja na skimu
hizo kuwa mbali na masoko jambo ambalo linapelekea kupanda kwa gharama za
usafishaji wa mazao kwenda kwenye masoko
na kukosekana kwa bei ya uhakika kitendo ambacho kinamuumiza mkulima
pamoja na kukosekana kwa vinu vya kuchakata nafaka
jambo ambalo linapelekea kukosekana kwa chakula cha mifugo kitokanacho na
mabaki ya nafaka hizo.
Awali akiongea katika kikao hicho kabla ya kutembelea skimu
hizo za umwagiliaji, Mhandisi wa kanda ya Umwagiliaji Dodoma inayohusisha mikoa
ya Dodoma, Singida na Simanjiro Bi Lucy Lema, alisema kuwa kutokana na kilimo
cha umwagiliaji kuwa chenye tija kwa
kuongeza pato la taifa na kuwepo kwa
uhakika wa chakula nchini, Serikali ina mikakati kabambe ya kuendeleza
kilimo hicho kwa kufanya upanuzi wa maeneo na kufanya tafiti
kabla ya ujenzi wa mabwawa, kufanyia ukarabati wa Miundombinu ya
umwagiliaji na kuendeleza skimu ndogo ndogo za umwagiliaji kupitia miradi mbali
mbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...