Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
IMELDA Marcos ambaye pia amewahi kuwa mke wa Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos  aliyetawala katika miaka ya 1965 na kutolewa kwa nguvu madarakani mwaka 1986 anashikilia rekodi ya kumiliki viatu vingi zaidi vinavyofikia jozi 3,000.

Mtandao wa Rappler wa nchini humo umeeleza kuwa Imelda amekuwa mpenzi wa viatu, vito vya dhahabu pamoja na nguo za nakshi ambapo baada ya kupinduliwa kwa mumewe aliacha maelfu ya jozi za viatu hivyo katika ikulu ya Malacanang na baadaye viatu hivyo vikapelekwa katika makumbusho maalumu iitwayo Makumbusho ya viatu ya Marikina.

Rappler imeeleza kuwa Imelda amekuwa anafahamika kwa mambo makuu mawili maarufu zaidi kwanza ni kuwa mke wa Rais dikteta wa nchi hiyo Ferdinand Marcos na kumiliki viatu vingi zaidi ambavyo vimeweka historia duniani kote.

Aidha imeelezwa kuwa jozi 3,000 za viatu zimethibitishwa na mamlaka husika licha ya viatu hivyo  kutoonekana bora zaidi kama vilivyotolewa katika Ikulu ya Malacanang mwaka 1986.

Rappler imeeleza kuwa viatu vya malkia huyo wa urembo kwa sasa  vinapatikana katika makumbusho ya Marikina ambako kuna jozi 720 huku jozi 253 zikiwa zimeuzwa na jozi 467 zimehifadhiwa.

Imeelezwa kuwa mamlaka iliamuru viatu hivyo vihamishiwe mjini mwaka 1996 ambapo FirstLady huyo aliandika na kueleza kuwa hakuwa na usemi.

Makumbusho hiyo iliyoanzishwa mwaka 2001 imekuwa ikihifadhi viatu hivyo huku ripoti  iliyochapishwa mwaka 2010 katika jarida la Gurdian ilieleza kuwa kuna zaidi ya makasha 150 ya nguo, vito, na viatu ambavyo vimeharibika kutokana na changamoto ya uhifadhi.

Makumbusho hayo ya viatu  yamekuwa yakitembelewa na wanafunzi na watalii na vimepangwa kwa rangi katika makumbusho hiyo ya Marikina.

Sehemu iliyopangwa viatu hivyo vimechukua sehemu kubwa ya ghorofa hiyo ikiitwa "Imelda's Footwear."

 Imeelezwa viatu  hivyo vimetengenezwa kutoka kampuni (brand) mbalimbali na hivyo vikiwemo viatu vya kuogea, vya kuvaa chumbani na vingi vikiwa vimetengenezwa nje ya Ufilipino ikiwemo nchini Taiwan na Ufaransa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...