Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akifungua rasmi mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF). Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika
Meneja wa Mafunzo ya Ukaguzi wa Kodi kutoka African Tax Administration Forum (ATAF) Caroline Mutayabarwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na ATAF ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019.
Baadhi ya Wakaguzi wa Kodi kutoka Mamlaka za Mapato Afrika wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF) ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019
Wakaguzi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF) ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya menejimenti ya TRA, wakufunzi na wakaguzi wa kodi mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na ATAF ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...