Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
RUFAA dhidi ya washtakiwa watatu kati ya wanne waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi bunju imeshindwa kuanza kusikilizwa kufuatia majalada ya warufani hao kuchanganywa.

 Hali hiyo imetokea leo Juni 13, 2019  baada ya wakili wa Serikali, Sadah Mohamed kuieleza mbele ya Naibu msajili wa Mahakama Kuu, Crecensia Kisongo kuwa, rufaa hiyo leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mwenendo wa kesi (proceedings) alionao siyo za mrufani aliyekuwa mahakani hapo, bali anayo ya mrufani Abrahamu Minga.
"Mheshimiwa, tunaomba muongozo wa mahakama ili kufahamu nini kifanyike, rufaa iliyoko mbele yako ni ya mrufani Konzo ambayo mi sijaipata na si ya mrufani Minga niliyonayo" ameeleza wakili Saada.
 Wakili wa warufani hao Profesa Abdallah Safari amedai kuwa  hati ya wito (summons) aliyonayo yeye ni ya washtakiwa watatu ambao ni, Yusuph Sungu maarufu kama Mayuku ambaye leo hakuwepo mahakamani, Juma Konzo na Abrahamu Minga.

 Rufani hiyo imeahirishwa hadi Juni 17 mwaka huu.

Mwezi Februari mwaka huu,  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwahukumu kifungo cha maisha washtakiwa wanane baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A ambapo 10 waliachiwa huru.

Waliohukumiwa ni Yusuph Sugu (40), Juma Kozo (32), Rashid Liwima (29), Baraka Nkoko (23), Abuu Issa (36), Abraham Mninga (23), Veronica Ephraem (32) na Ramadhan Said (22).

Walioachiwa huru ni Mrisho Majaliwa (30), Hamis Ndege (37), Seleman Gwae (33), Menge’nya Anthony (28), Rehema Hussein (32) Rajabu Ally (25), Ally Athuman (24), Amina Matipwili (33), Gubila Temba (51) na Mariam Honza (44).

Wanadaiwa Julai 10, 2015. Walichoma kituo cha polisi ambacho ni mali ya umma jambo ambalo ni kosa la kisheria.
 Warufani, Juma Konzo na Abrahamu Minga wakielekea mahakamani kusikiliza rufaa yao waliyokata baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi bunju, hata hivyo Rufaa hiyo imeahirishwa kufuatia majalada yake kuchanganywa.
Ndugu wa warufani hao wakimsikiliza wakili wa warufani hao, Profesa Abdallah Safari baada ya kesi hiyo kuahirishwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...