Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) wanaendesha mkutano wa siku tano kwa nchi wanachama wa IAEA kanda ya Afrika, zinazodhibiti usalama wa mionzi.

Lengo kuu la mkutano uliohudhuriwa na jumla ya washiriki 27 kutoka Botswana, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Misri, Ethiopia, Gabon, Ghana, Madagascar, Malawi, Mali, Nigeria, Sudan na Tanzania ni kujadili  na kutoa miongozo kulingana na viwango vya usalama kwa wasimamizi wa nchi za wanachama wa Afrika juu ya utoaji wa leseni na ukaguzi wa shughuli za mzunguko wa uzalishaji wa madini ya urani.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Injinia John Ben Ngatunga alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo katika hotel ya SG Premium Resort ya Jijini Arusha hivi leo,  amewataka washiriki wote kufanya majadiliano ambayo yatasaidia kuelewa miundombinu iliyopendekezwa ya sheria na udhibiti wa madini ya urani na majukumu ya washirika wengine wa udhibiti katika ngazi za kitaifa na kimataifa.


Imetolewa na;

Peter G. Ngamilo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...