Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akionyesha bunduki aina ya Ak -47 pamoja na risasi 20 zilizokamatwa jana katika misitu ya milima ya Digodigo Tarafa ya Sale wilaya ya Ngoronroro.
Na Vero Ignatus,Arusha
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuwawa katika majibizano na polisi eneo la Digodigo ,Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro
Akizungumza na waandishi wa habari jana , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana alisema ,majambazi hayo yalikuwa na bunduki aina ya Ak -47 pamoja na risasi 20
Amesema majibizano hayo yalichukua zaidi ya dakika 75 huku wenyeji wakishuhudia mirindimo ya risasi ambapo tukio hilo liketokea jana saa 3:00 asubuhi kwenye msitu wa Digodigo Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro
Aliwataja waliokufa kuwa ni Kulima Albart (35) mkazi wa kijiji cha Mholo na Hashim Nginodya(28)mkazi wa Digodigo ambapo miili yao umehifadhiwa hospitali ya Digodigo
Amesema watu hao wanaosadikiwa ni majambazi walikuwa wakitafutwa muda mrefu kwa matukio ya unyang'anyi na kuteka watalii
"Majibizano ya risasi yalichukua dakika 75 pia baada ya majibizano walikutwa na risasi 20 pamoja na bunduki aina ya Ak-47"
Sambamba na hayo Kamanda Shana amesisitiza kuwalinda wafanyabishara wote wa Mkoa wa Arusha na kutoa rai walipe kodi ikiwemo kufuata taratibu za kisheria zilizopo katika kufanya shuguli zao
Natoa onyo kali kwa wale wote wakwepa kodi kuhakikisha wanaliodi ili wasije kukumbana na mkono wa serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...