Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Sudan Kusini  Ndugu Paul Mayomu atembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR kipande cha Daresalaam  - Morogoro, Ziara hiyo imefanyika hivi karibuniJune , 2019. 

Aidha, katika  ziara hiyo iliongozwa na mwenyeji wake  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, walipata fursa ya kuona maendeleo na hatua tofauti za ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR ukiwemo ujenzi wa stesheni kuu ya Daresalaam, madaraja, na utandikaji wa reli unao endelea maeneo  ya vingunguti jijini Dar Es Salaam. 

Waziri Mayomu ameipongeza Tanzania kwa kuamua kujenga Reli ya Kisasa - SGR ambayo ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi, viwanda na biashara katika Taifa na nchi jirani. 

Hata hivyo, Waziri Mayomu ameeleza kuwa reli hii itakapo kamilika itakuwa chachu ya maendeleo kwa nchi zote mbili pia itadumisha uhusiano katika sekta ya uchukuzi, viwanda na biashara kati ya Tanzania na Sudan ya Kusini.

Kwa upande wake, Waziri  Kamwelwe amempongeza waziri Mayomu kwa kuja Tanzania ambayo ni heshima kwa Taifa na kujionea maendeleo yanayofanyika katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi katika ujenzi wa reli ya kisasa ambayo ni chachu ya maendeleo baina ya nchi hizo mbili.

Waziri  Kamwelwe ameahidi kudumisha uhusiano kupitia reli ya kisasa hasa katika sekta ya viwanda, biashara na uchumi.
  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...