Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, imeelezwa kuwa, mtoto Naomi John (7) alifanyiwa ukatili uliopitiliza na bibi yake uliopelekea kifo chake.

WP 2265 Ditectivu Sajenti Mgeni amedai hayo leo mbele ya Msajili Pamela Mazengo alipokuwa akitoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Esther Lyimo ambae anatuhumiwa kumuua mjuu wake Naomi John Machi 25, 2017.

Akiongozwa na Wakili Cecilia Mkonongo kutoa ushahidi wake, WP Mgeni amedai, Machi 25,2017 alipigiwa simu na mkuu wa upelelezi Mbagala ambae alimtaarifu juu ya tukio la mauaji maeneo ya Tuangoma Kigambo na kumtaka alifanyie kazi.

Amedai Machi 26, 2017 alipoingia ofisini alilichukua jalada hilo na kulisoma ndipo akagundua kuwa kuna washtakiwa watatu katika kesi hiyo ambao wote ni wanawake. 

Ameendelea kudai kuwa, baada ya kulisoma jalada lile alienda eneo la tukio huko Tuangoma akiwa ameongozana na mtoto wake Victoria pamoja na askari Aloyce, ambapo baada ya kufika tulipogonga wakatoka vijana wawili ndani mmoja alionekana kuwa na miaka 7 na mwingine 13 hadi 14.

"Niliwauliza mama yupo mtoto huyo wa miaka saba (jina limehifadhiwa) akasema hayupo, ameenda wapi? ameenda hospitali, na baba je hayupo pia, wakati namuhoji mtoto yule shingoni alionekana kuwa na alama, nikamuuliza tena akasema ameumia, nikamuuliza na hapa kifuani hakijubu kitu alionekana kama anaona aibu kuongea, lakini nilipoendelea kumuangalia nikamuona mkononi anakidonda na kichwani alikuwa amevimba.

Ameendelea kudai kuwa, nilipomuuliza akamjibu kuwa mama yake mdogo alimpiga na fimbo, akadai, akaamua kumfunua shati  ndipo alikuta mwili mzima mtoto anamajeraha na makovu yaani mwili mzima alionekana kama ngozi ya kenge.

" Nilipomuangalia yule mtoto nilibaini hata yule aliyekufa atakuwa amefanyiwa ukatili kama huyu isipokuwa huyu hajafa".Nilimjulisha afande Walelo akasema niendelee na upelelezi ila mtoto yule niliyemkuta na majeraha niende nae kituoni.

Ameendelea kudai kuwa, alipotoka pale,  alienda kwa majirani ambapo alimkuta jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi ambae alipomueleza kuwa Naomi amefariki alilia sana, ndipo yeye akafanya kazi ya kumbembeleza  kabla ya kumuhoji.

"Mwanahamisi alinieleza kuwa, wale walikuwa ni majirani na mara nyingi alikuwa akimuona Esther akimpiga Naomi, Naomi alikuwa mtoto mdogo lakini alikuwa anafanya kazi za mtu mkubwa, ambapo alienda na kumuuliza mbona watoto unawapiga sana ndipo hapo ukawa mwanzo wa uhasama akawa akimsalimia haitiki.

Nae Koplo Joyce akitoa ushahidi wake mahakamani hapo amedai aliitwa kwenda Hospitali ya Temeke baada kupata taarifa kuwa kuna mtoto amefikishwa pale hospitali  akiwa Katika hali ambayo siyo nzuri na kwamba Dk. aiyempokea alibaini kuwa mtoto yule alishakufa masaa kadhaa nyuma Ila waliompeleka wanadai kuwa ni mgonjwa na walipomkagua alikuwa na majeraha ambayo siyo ya kawaida.


Amedai, alipomuhoji mshtakiwa majeraha na makovu yaliyokutwa kwenye mwili wa marehemu yalisababishwa na nini alimjibu " Mimi huwa nampiga pale anapokosea kwa utukutu wake"  nilipowauliza watu aliofuatana nao kumpeleka mtoto Naomi hospitali Victoria na Jackline  vitendo vya ukatili alivyokuwa anafanyiwq huyo mtoto hawakuwa wakiviona? Walimwambia "tulikuwa tunaviona ila mama ni mkali sana hata ukiongea nae haelewi".

Kwa upande wake Inspekta Salma Sechenzo akitoa ushahidi wake alidai wakati anamchukua mshtakiwa maelezo ya onyo alikiri kumchapa mtoto Naomi na kumfinya mara kwa mara na kila mara alopokuwa akimpiga alikuwa akirejea maeneo yale yale yenye majeraha.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, (Ijumaa) Mtoto wa miaka tisa aliezeza mahakamani hapo jinsi mama yake mdogo, Esther Lymo (mshtakiwa) alivyowatesa hadi mwenzake Naomi John (9)akapoteza maisha.

Mtoto huyo alidai alikuwa akiishi Dar es Salaam na mama yake mdogo ambaye pia ni mama yake wa ubatizo pamoja dada zake.
"Tulikuwa tunaishi pamoja na Junior, dada Sia na Naomi, Namfahamu Naomi John tulikuwa tunakaa naye pale pale, lakini yeye amezikwa.
Wakili:Naomi yuko wapi.
Mtoto:Amezikwa alipigwa mpaka akafa.
Wakili; Alipigwa na nani.
Mtoto: Alipigwa na mama yule pale.
Wakili:Alifanya nini akapigwa.
Mtoto:Alimwaga maji yakasambaa nyumba nzima akaambiwa ayafute.
Wakili:Aliyafuta.
Mtoto:Alianza kuyafuta, alipofika akafika sehemu akagoma kuendelea kufuta.
Wakili;Alipokataa ikawaje.
Mtoto;Mama mdogo akaanza kumpiga na fimbo ya mpera, alimpiga... zilikuwa fimbo nyingi hadi ikabakia moja.
Wakili;Elezea ilivyokuwa.
Mtoto;Mamdogo alimng'ata mgongoni akamnyanyua juu kisha akamwachia, akamweka katika maji akamtoa na kumweka barazani, akamwagia chai ya moto.
"Naomi alipoachiwa alianguka chini, alikuwa kachoka, akamchukua akampeleka ndani, alimpeleka bafuni akamtoa akaenda kumlaza kitandani, akamwashia feni, Naomi alikuwa kachoka sana.
"Aliniita mamdogo akanituma dukani nikanunue unga wa kumkologea uji, niliporudi dukani nilimkuta Naomi anatoka povu puani.
"Mama alienda kununua dawa, aliporudi alimkuta Naomi kafariki,"alidai.
Wakili:Ulijuaje kama Naomi kafariki.
Mtoto: Nilijua sababu wakina dada niliwaona wanalia, wakamchukua Naomi wakampeleka hospitali.
Alidai alibaki nyumbani na Junior, akafika mjomba wake Hamza akampa hela akanunue soda lakini naye mwilini alikuwa na makovu yaliyotokana na kupigwa na mama mdogo.
"Askari walinichukua wakanipeleka hospitali, nilikaa hospitali kesho yake nikapelekwa Kituo cha kulelea watoto yatima, nikiwa hospitali madaktari walinidanganya kwamba Naomi hajafa ili nisilie, waliniambia nitamuona lakini sijamuona tena,"alidai na kuongeza kwamba alioneshwa kaburi la Naomi.
Alipotakiwa kueleza kaburi ni kitu gani alisema ni shimo 
Mtoto huyo alinalowekwa jeneza lililotengezwa kwa mbao.
Mtoto Naomi hakuwa anakosa mara zote, mama mdogo alikuwa akimpiga hata yeye na ubapa wa panga fupi na kumfinya kwa kutumia kucha na kisu cha kukatia ugali.
Shahidi huyo aliiinesha mahakama kovu katika mkono wake lililotokana na kupigwa na ubapa wa panga.


Aidha shahidi wa pili, Daktari kutoka Temeke, DK.Abdulkarim Aljabir alidai alimpokea Naomi baada ya kuletwa na mshtakiwa Esther Lymo akidai malaria ilipanda kichwani naye alipewa taarifa ndio akamfata na kumkimbiza hospitali.
"Nilimsaidia kumfungua mgongoni mgonjwa, alikuwa amelegea sana, nikamlaza katika kitanda na kuanza kumchunguza.

"Nilipomchunguza nilibaini baadhi ya vitu haviko sawa, mapigo ya moyo hayakuwepo, msukumo wa damu haukuwepo macho na mdomo vilikuwa wazi, mboni ya jicho ilitanuka, ishara hiyo ilinijulisha kwamba alifariki zaidi ya saa nne zilizopita.

"Tulipomchunguza zaidi na madaktari wenzangu tulibaini, kichwani kulikuwa na uvimbe mkubwa sio wa muda mrefu uliotokana na kuvilia kwa damu kwa sababu ya kupigwa na kitu kizito kisichokuwa na ncha.

"Mdomo wa Naomi ulikuwa unakosa meno matatu yaliyoondolewa bila kufuata utaratibu wa ung'oaji wa meno hali iliyosababisha majeraha kwenye vizi na ulimi.

"Kifuani kulikuwa na majeraha mapya na ya zamani, mkono wa kulia ulivunjika mara mbili, bega la kulia liliteguka, tumbo lilikuwa halina chakula kabisa zaidi ya gesi, sehemu za siri kote kote kulikuwa na michubuka, mapaja yote mawili yalikuwa na vidonda na alama za kuungua moto,"alidai.

Daktari alitaja sababu ya kifo cha Naomi ni majeraha kichwani, bakteria katika mwili wake kwa kiwango kikubwa kisichotibika na alipata maumivu makali yaliyosababisha kushindwa kustahmili. Kesi hiyo inaendelea kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...