Na Charles James, Michuzi TV
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Izava, Kata ya Segala (Tarafa ya Itiso - Wilaya ya Chamwino) kwa tiketi ya CHADEMA Sokoine Mndewa jana Julai 12 alitangaza rasmi kuhamia Chama cha Mapinduzi na kujivua nyadhifa zote ndani ya chama hicho.
Uamuzi huo ulifikiwa na kiongozi huyo kupitia kikao cha Afisa Tarafa ItisoRemidius Emmanuel alipokutana na viongozi wa chama na serikali kata ya Segala wakati wa majadiliano ya pamoja juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kata hiyo.
Akichangia mada katika kikao hicho Sokoine mbali na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi dhamira ya kuhamia CCM.
Sokoine amesema kuwa sababu za kujiunga na Chama cha Mapinduzi ni pamoja na tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2014 hadi sasa amekuwa akikosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wake wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Pia amesema kuwa amejiunga na CCM baada ya kufurahishwa zaidi na kasi ya utendaji kazi wa Rais Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
"Rais Magufuli ametufilisi yale yote ambayo tumekuwa tukiyapigia kelele miaka yote, sote ni mashahidi wakati wote Chadema ilisisitiza kushughulikia Mafisadi, nidhamu katika utumishi, kuwachukulia hatua za haraka pasipo upendeleo wale wote wanaotoa na kupokea rushwa na bado tunaendelea kushuhudia mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya tano katika Sekta ya Afya, elimu, na madini, Sasa ninabaki huku kufanya nini? ni mwendawazimu pekee anaweza kupuuza mafanikio haya" ameeleza Sokoine.
Amesema kuwa ameamua rasmi kujivua uanachama wake ndani ya Chadema na kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa tiketi ya Chadema na kujiunga rasmi na CCM, na kuomba wanipokee.
Aidha amesema hatua yake hiyo ni maamuzi yake binafsi pasipo shinikizo lolote.
"Nimefikia uamuzi huu nikiwa na akili timamu pasipo kushauriwa na mtu yeyote na nipo tayari kujiunga na CCM kama mwanachama wa kawaida" ameeleza.
Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Chamwino Sostenes Tumbo amempongeza kiongozi huyo kwa uamuzi sahihi na kueleza kwamba anakaribishwa CCM huku akiwahimiza wanachama wote kumpatia ushirikiano.
Mapema akizungumza katika kikao hicho Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel alisema ataendelea kufanya vikao vya mara kwa mara baina ya viongozi wa Chama Tawala na Serikali katika tarafa yake hatua ambayo anaamini inatoa fursa ya majadiliano ya pamoja katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
"Lazima mtupime na kujiridhisha juu ya Utekelezaji wa ilani ya CCM, mimi kama kiongozi mkuu wa Tarafa ya Itiso pamoja na viongozi walioko chini yangu imani yetu kubwa ni kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatekeleza vema Ilani ya Chama cha Mapinduzi" alieleza.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Diwani wa kata ya Buigiri Keneth Yindi, Diwani wa Kata ya Segala Hemed Sablugo, Diwani wa Viti Maalum Mariam Chisonjela, Kamati ya Utekelezaji UWT (W) na Mwakilishi wa Mbunge jimbo la Chilonwa Josia George.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava kwa tiketi ya Chadema Sokoine Mndewa (Kushoto) akikabidhi kadi yake kwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Segala ndugu Benjamin Sadala.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava (Wilaya ya Chamwino) kwa tiketi ya Chadema Sokoine Mndewa akila kiapo mbele ya Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Chamwino ndugu Sostenes Tumbo (Kulia) mara baada ya kujiuzulu wadhifa wake na kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi.
AfisaTarafa Itiso, Remidius Emmanuel alizungumza na viongozi wa Chama (CCM) na Serikali wakati wa majadiliano ya pamoja juu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kata ya Segala.

Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava Mkoani Dodoma kupitia tiketi ya Chama
hicho, Sokoine Mndewa akizungumza na wananchama wa CCM (hawapo pichani)
mara baada ya Kujiuzulu nafasi zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi(CCM).
Baadhi
ya viongozi mbalimbali walioshiriki kikao hicho kilicholenga kujadili
utekekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kata ya Segala na
kupelekea aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava kwa tiketi ya
Chadema Sokoine Mndewa kutangaza rasmi kujiunga na CCM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...