Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imetoa amri ya 
kukamatwa raia mmoja wa Russia Vadim Burin ili afikishwe mahakamani hapo kujibu mashtaka nane yanayomkabili yakiwemo ya kuingilia mawasiliano ya kielectroniki na kuisababishia Serikali ya Tanzania na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA hasara ya milioni 41.

Mshtakiwa Burin ambae pia ni mfanyabiashara anayeishi Morovania nchini humo anashtakiwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na Mtanzania, Msafiri Msayi aliyesomewa mashtaka yake pasipokuwepo na mshtakiwa namba moja (Burin) mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Salum Ally baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Monica Mbogo kuiomba mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo na mahakama ikaridhia.

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya Msayi, Wakili wa Serikali Batilda Mushi 
akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai Burin na Msayi wanatuhumiwa kwa mashtaka nane,waliyoyatenda kati ya Mei, 15 hadi Juni 10 mwaka huu.

katika shtaka la kwanza, inadaiwa katika siku na tarehe zisizofahamika jijini Darces Salaam, washtakiwa walikula njama ya kutumia mtandao wa njia ya udanganyifu.Washtakiwa wandaiwa Mei 15, mwaka huu wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere waliingiza vifaa vya kieletroniki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo ni,one voice over internet protocol (VOIP) na Gateway model GOIP-8 yenye kumbukumbu namba GOIP8MCDRM17033127.

Pia MAC ADR383F10048B10, 383F10048B11,8channel, one VOIP Gateway S/N 8M2ARMV51800553, MAC adress 383F105CBD6, 383F1005CBD7, Eight 
channel, one VOIP Gateway S/N SMB32T18110540, MAC address 
383F1005108,388F1005DE09 bila ya kuwa na leseni kutoka TCRA.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa bila uhalali wowote walisimika mifumo ya kieletroniki bila kuwa na leseni ya TCRA. Katika shtaka la nne, imedaiwa, kati ya Mei 15 na Juni 10,mwaka huko Sea Cliff, Masaki, Wilaya Kinondoni, washtakiwa walitumia vifaa vya mawasiliano vya kieletroniki ambavyo waliviunganisha kwa lengo la kupokea na kutoa mawasiliano bila kuwa na kibali cha TCRA. 

Katika shtaka la tano, washtakiwa wandaiwa siku na mahali hapo, waliendesha mtambo wa mawasiliano kwa lengo la kupokea na kutoa mawasiliano ya kimataifa bila kuwa na leseni.

Aidha kwa lengo la kukwepa kodi, washtakiwa wanadaiwa kukwepa malipo 
ambayo yanatolewa katika huduma ya kutoa mawasiliano ya kimataifa ambapo bila kujali walisambaza mawasiliano hayo kwa kuunganisha mawasiliano ya kimataifa huku pia washtakiwa hao wanadaiwa kutumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa, ambapo za halotel zilikuwa 173 na Vodacom zilikuwa 37. 

Katika shtaka la mwisho, washtakiwa wanatuhumiwa kuisababishia Serikali na TCRA hasara ya Sh.milioni 41.7. Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya 

kusikiliza shauri hilo na kesi imeahirishwa hadi Agosti Mosi, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...