Na,Jusline Marco.Arusha

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Arusha kupitia chama cha mapinduzi Catherine Magige amekabidhi mashine ya kukoboa na kusaga yenye thamani ya shilingi milioni 3 na laki 5 kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kimaendeleo za chama hicho katika Wilaya ya Arumeru.

Akikabidhi mashine hiyo kwa viongozi wa UWT Wilaya ya Arumeru Mbuge Magige amewataka viongozi hao kukemea vitendo viovu vinavyoendelea katika kata zao vikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na unywaji wa pombe uliokithiri katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wilayani humo Bi.Angela Mvaa akitoa ufafanuzi wa idara hiyo kwa wanawake hao amesema kuwa ili kuweza kuwa na jamii yenye maadili ni lazima wanawake wawe chachu ya mabadiliko katikati ya jamii zao.

Aidha amesema kuwa katika Wilaya hiyo vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono vimekithiri katika Kata ya sokoni 2,olmotonyi pamoja na oltrument na vimeonekana kushika kasi huku baadhi ya wazazi na wazee wa uko kuwa visababishi vya kumnyima mtoto haki zake za msingi kwa kumaliza matukio hayo kimila huku wengine wakikataa kutoa ushirikiano katika vyombo husika.

Ameongeza kuwa wapo baadhi ya watu huzuia kupatikanaji wa haki za mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kingono kwa kutokutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama huku wengine wakisuluhisha matatizo hayo kwa njia ya kimila.

Hata hivyo hivi karibuni kumetokea tukio katika kata ya Olorien kijiji cha Olosiva baada ya mzazi aliyefahamika kwa jina la Aristerico Silayo kumbaka mtoto wake Angel Aristerico akiwa na umri wa miaka 11 tangu mwaka 2016 mpaka sana kitendo ambacho wanakijiji wa kijiji hicho wamekilaani vikali kutokana na mzazi huyo pamoja na kukutwa na hatia ya kutenda kosa hilo aliachiwa huru na mahakama ya Hakimu mkazi Arusha,M Mwankunga kupitia kifungu cha 235 cha Sheria ya makosa ya jinai.
 Mbunge wa Viti maalum Catherine Magige akikabidhi mashine ya kusaga na kukoboa kwa chama cha UWT Wilaya ya Arumeru zitakazo wasaidia katika uongezaji wa kipato katika chama chao
Mbunge Magige akikabidhi bati hamsini kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Charles Mahera,akiunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...