Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally na kulia ni Mkurugenzi Mkuu Takukuru, Diwani Athuman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifurahia jambo katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally, akiteta Jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius NyerereJijini Dar es Salaam,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika akufuatilia mijadala mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Takukuru, Diwani Athuman akisisitiza jambo wakati wa kuwasilisha Mada yake kuhusu Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya Rushwa, katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa lililofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Takukuru, Diwani Athuman akiwasilisha Mada mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maanajimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Kapt.Mstaafu George Mkuchika, kuhusu Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya Rushwa, kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam huku kauli Mbiu yake ikiwa ni ‘Usindikazi wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda’ 
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
…………………..
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika amesema Tanzania inaendelea kupata heshima kubwa katika Jumuiya ya Kimataifa katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa kutokana na mshikamano na nguvu ya pamoja iliyopo katika vyombo na taasisi zinazosimamia utawala bora nchini.

Akizungumza katika kongamano la siku maalum dhidi ya rushwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Julai 3, 2019) Waziri Mkuchika alisema utafiti uliofanywa na taasisi hizo zimesifu juhudi za zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya mfano katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa.

Mkuchika aliasema taasisi hizo zikiwemo MO Ibrahim, Transparency International, APRM na taasisi nyingine kubwa duniani zinazosimamia masuala ya utawala bora zimefanya utafiti na kusifu juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo tafiti mbalimbali zimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili nyuma ya nchi ya Rwanda.

Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kuweka mkazo na msukumo katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo taasisi zote zinazosimamia masuala ya utawala bora zimekuwa zikiunganisha nguvu ya pamoja na kulifanya suala la rushwa sasa kuwa na nguvu na msukumo mpya wa mapambano katika jamii.

“Kwa sasa vyombo vyetu vyote serikalini si TAKUKURU pekee bali pia polisi, tiss (usalama wa taifa), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ICAG) na vingine vyote, vimeendelea kuunga katika kusimamia masuala ya utawala bora na hili limeleta msukumo na hamasa mpya katika vita dhidi ya rushwa hapa nchini” alisema Waziri Mkuchika

Akizungumzia rushwa katika sekta ya viwanda na biashara, Waziri Mkuchika alisema Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali katika kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likiathiri sekta binafsi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika alisema rushwa katika sekta biashara imekuwa ikiathiri sana masuala ya uwekezaji wa kigeni, ambapo eneo lililonyesha kutawala kwa rushwa ni katika eneo la utoaji wa vibali na leseni kutoka katika taasisi na idara muhimu za serikalini na hivyo serikali imeendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa kwa wawekezaji na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.

Akifafanua zaidi Mkuchika anasema kutokana na serikali kutambua mchango wa sekta ya viwanda na biashara katika kukuza uchumi na uzalishaji wa ajira nchini ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali imekuwa ikifanya marekebisho mbalimbali ya sheria na sera mbalimbali ambazo zimekuwa ni sehemu ya mianya ya rushwa nchini ikiwemo eneo la kodi.

“Kutokana na kudhibiti rushwa kwa sasa kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya mwezi yameweza kuongezeka kutoka Tsh Bilioni 800 kwa mwezi hadi kufikia Tsh trilioni 1.3 hii inaoyesha kuwa kulikuwa na maeneo ambayo kulikuwa na uvujaji wa mapato ya serikali kulikochangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athumani alisema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kupitia Mpango Mkakati dhidi ya mapambano ya rushwa (NASCAP III) ili kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya rushwa yanapata mafanikio nchini.

Anaongeza kuwa kupitia NASCAP III, ofisi yake imeendelea kutekeleza masuala mbalimbaliu ikiwemo kufanya tafiti kubaini ukubwa na kiwango cha rushwa nchini, kupokea maoni, kutoa elimu kwa umma kupitia makongamano, rushwa pamoja na kufanya uchunguzi na kufungua mashtaka kwa watu mbalimbali wanaopatikana na hatia dhidi ya rushwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...