Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

SERIKALI itawasilisha orodha ya tozo zote 49 zilizofutwa ambazo zilikuwa ni kero kwa wajasriamali na wafanyabiashara ili waweze kuzielewa na hivyo kulipa kodi bila ucheleweshaji..

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Viwanda na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya shughuli za kibiashara kutoka SIDO pamoja na mkopo kwenye Viwanja vya Sido mkoa wa Arusha .

Waziri,Manyanya,amesema serikali kwenye kikao kilichofanya na wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam,hivi karibuni ilifuta utitiri wa tozo zilizokuwa zikilalamikiwa na hivyo kuwapunguzia mzigo wafanyabiashara na wajasiriamali nchini

Amesema kuwa hivi sasa serikali ipo katika ujenzi wa Viwanda na hivi karibuni alikutana na Waziri wa Uholanzi lengo ni kuwajengea mazingira ya uwezeshaji wafanyabiashara nchini waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi na anatarajia kuona kila mmoja anashiriki .

Waziri Manyanya,amesema Sido imepiga hatua katika teknolojia na jukumu lililopo sasa ni kuendelea kuhamasisha na kuwaomba wajasriamali wazidishe ubunifu ,wazalishe bidhaa zenye ubora zaidi, watumie mitandao kutafuta masoko .

Amewasisitiza wajasriama na wafanyabiashara kutumia lugha za zinazoeleweka za Kiswahili kwa ajili ya soko la ndani na kiingereza kwa ajili ya soko la nje ili kumuwezesha mlaji kuelewa aina ya bidhaa anazotumia.

Amesema wizara imejipanga katika kanda saba kwa ajili ya kuwasikiliza wadau na anatembelea nchi nzima ili kuzungumza nao na kwa kuanza ameanzia Arusha na ameenda Manyara .

Awali Meneja wa Sido mkoa wa Arusha Nina Nchimbi, amesema hivi sasa SIDO inaanza kuwafundisha wajasriama elimu ya haki miliki kwa ajili ya kulinda biashara zao kwani wengi wao hawana elimu hiyo.

Kuhusu Vifungashio vya bidhaa za wajasiriamali Nchimbi,amesema hilo ni tatizo hivyo akakiomba kiwanda cha Kioo Limited cha Dar es Salaam kuzalisha vifungashio vingi ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani.

Ameongeza kuwa Sido katika kazi zake imekuwa ikishirikiana na taasisi zingine za serikali zikiwemo TRA, TMDA, katika kutoa elimu ili kuwaondolea wananchi usumbufu lakini kuna baadhi ya watumishi wa tasisi hizo wanalalamikiwa .

Wakichangia kwenye kikao hicho Wadau hao wameilalamikia ofisi ya mkemia mkuu kuwa ina urasimi hivyo kuwa ni kikwazo katika shughuli zao

Taasisi nyingine iliyolalamikiwa ni pamoja na Mamlaka ya mapato mkoa wa Arusha kuwa kuna baadhi ya watendaji wake ni kikwazo,ambapo kuna kulindana na hivyo kusababisha wajasriamali 67 waliopatiwa mafunzo na SIDO kushindwa kuanzisha Viwanda.

Aidha wameiomba serikali kuongeza fungu kwenye mfuko wa SIDO ili waweze kupata mikopo mikubwa ya fedha badala ya sasa ambapo kikomo cha mikopo inaotolewa na SIdo ni shilingi milioni tano tu.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Viwanda na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya shughuli za kibiashara kutoka SIDO .
 Meneja wa shirika la Sido mkoa wa Arusha,Nina Nchimbi akizungumza katika mkutano huo wa wajasiriamali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...