Anaadika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Karagwe.

Serikali kupitia Wizara ya Maji  ipo mbioni kuanza kujenga miradi ya Maji katika Miji 28 Nchini Tanzania ukiwemo Mji wa Kayanga ambapo Waziri mwenye dhamana Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imekwisha chukua mkopo nafuu kutoka  Serikali ya India  Shilingi Trioni 1.2 na zabuni ya mradi huo mkubwa itatangazwa Septemba,  na kukamilika kwa Mradi  huo kutatatua kero ya Maji ndani ya Miji ya Kayanga na Omurushaka zaidi ya 100%.

Waziri Mbarawa kabla ya kuelekea Missenyi akitokea Muleba amezindua mradi wa Maji wa Izigo wenye gharama zaidi ya  shilingi Milioni 600  Na mradi huo tayari unafanya kazi huku akifurahishwa na Kamati ya Mradi huo kukusanya kiasi cha shilingi Milioni sita mpaka sasa yakiwa ni mauzo ya Maji.

Akiwa Wilayani Karagwe Waziri ametembelea chanzo cha Maji cha Kayanga  ambacho ni Mradi unaosimamiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Bukoba (BUWASA), wenye gharama ya Shilingi Bilioni 1.8 ukiwa  umekamilika kwa 75@%  huku BUWASA wakiahidi kufikia Mwezi Oktoba utakuwa umekamilika 100%.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maji Profesa Mbarawa ameagiza kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Karagwe kuwakamata watu watatu wanaosemekana kuwa ni Viongozi wa kamati ya Maji ya Mradi wa Maji Chabuhora Kata Bushangaro, kwa kuhujumu mradi huo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kukusanya pesa ya mauzo ya Maji katika mradi huo.Waziri Mbarawa tayari  kamaliza ziara hiyo katika Wilaya ya Missenyi na Karagwe na sasa yupo Kyerwa.
 Waziri Mbarawa akipanda Mti rafiki na maji kama ishara ya uzinduzi wa kampeni ya kutunza chanzo cha Maji Izigo
Pichani Waziri Mbarawa akizindua kampeni ya Utunzaji wa Chanzo cha Mradi wa  Maji Izigo kwa kushirikiana na Mhandisi Luyango Mkuu wa Wilaya Muleba.
Waziri Mbarawa akijiridhisha katika moja ya DP 23 za mradi wa Maji wa Chabuhora ambapo alielezwa kuwa hazitoi maji.
Mradi wa Maji unaotumia teknolojia ya Polyglue kama unavyoonekana pichani, eneo la Kyaka Darajani Wilayani Missenyi

Mradi wa Maji wa Chabuhora Wilayani Karagwe ambao makusanyo yake hayajulikani na kupelekea Waziri Mbarawa kuagiza wahusika kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Pichani Waziri Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam akiwa katika Mradi wa Maji Kayanga unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Bukoba (BUWASA) Mara baada ya Kuwasili Wilayani Karagwe.
Pichani Waziri Mbarawa akikagua mradi wa Maji unaotumia teknolojia ya Polyglue ambapo Maji kutoka Mto Kagera huwekewa mbegu za Maharagwe ili kusaidia kuondoa mchanga na vumbi, Wilayani Missenyi chini ya ufadhili wa Shirika la JICA la Nchini Japan.
Pichani ni wakazi wa Kishao Wilayani Karagwe wakiendelea kufurahia huduma ya Mradi wa Maji licha ya Kukamilia asilimia 75, kama walivyokutwa na kamera yetu.
Waziri Mbarawa akiimba pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya CCM Wilaya ya Missenyi, alipopita kuwasalimia akiwa Ziarani Missenyi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...