Na Charles James, Michuzi TV

BENKI ya Posta Nchini TPB leo imekabidhi gawio la Shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali pamoja na wanahisa wengine kama faida ambayo wameipata kutokana na shughuli zake ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Gawio hilo limekabidhiwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango leo katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea gawio hilo, Waziri Dk Mpango ameipongeza Benki ya TPB kwa kuendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takribani 50 yaliyopo nchini.

" Kwa kweli ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo Benki ya Posta imelifanya, nitoe shukrani za dhati kwa Uongozi wa Benki hii kwa gawio hili la Bilioni moja ambalo mmelitoa kwa Serikali, hii ni mara ya pili mfululizo mmetoa gawio hili na hakika mnastahili pongezi.

" Kutoa kwenu gawio hili kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki hisa kwenye Benki yenu," Amesema Dk Mpango.

Dk Mpango pia ametoa wito kwa Taasisi zingine za umma zinazotaka huduma za kibenki kote nchini na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Dk Edmund Mndolwa amesema Benki ya TPB imefanya vizuri kwa mwaka jana kwa kupata faida ya Shilingi Bilioni 17 na hivyo kuweza kutoa gawio la Shilingi Bilioni Moja kwa wanahisa zake na Serikali.

" Najisikia daraja kusimamia Benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki yaliyopo sokoni, ni matumaini yetu kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dk Magufuli katika kuifanya Tanzania inafikia uchumi wa kati," Amesema Dk Mndolwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...