Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
DAKTARI bingwa wa uchunguzi wa vifo vyenye utata na magonjwa mbali mbali wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Innocent Mosha ameileza mahakama kuwa kifo cha marehemu Bahati Hussein kilisababishwa na majeraha yakiyokutwa sngoni kwake baada ya pingili zake mbili kutenguka.

Akiongozwa na wakili wa serikali,  Erick Shija kutoa ushahidi wake leo, Julai 9 2019, shahidi huyo amedai, alipoufanyia uchunguzi mwili wa marehemu aligundua pia kulikuwa na mvilio wa damu kuzunguka pingili zake za Shingo na mapafu yake yalikuwa yamejaa damu na hewa.

Katika kesi hiyo, Godfrey Samwel maarufu kama Nkwabi anadaiwa kumuua kwa makusudi make wake Bahati Hussein.

Mbele ya msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo, Dr. Mosha ambae ni shahidi wa sita na wa mwisho katika kesi hiyo amedai, Juni 23,2012   akiwa kazini, alipokea amri kutoka jeshi la polisi Stakishari lililomtaka  kufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Bahati Hussein ambae walikuwa wanahisi kuwa ameuwawa kwa kupigwa.

 Akadai, baada ya kupokea amri hiyo, alipata mashahidi wawili  walioenda pamoja na mpelelezi kwa ajili ya kumtambua marehemu ambao ni Muhidin hamisi na Maxmillian ambapo baada ya zoezi La  utambuzi kabla ya kuanza kufanya uchunguzi alipata maelezo mafupi kutoka kwa mpelelezi E 1279 ditektivu Koplo Peter.
Amesema, alifanya uchunguzi katika sehemu ya nje ya mwili wa marehemu na ndani ambapo katika sehemu ya nje mwili wa marehemu ulikutwa na michubuko kidogo katika sehemu ya shingoni huku macho yake yakiwa na mivilio midogo midogo ya damu na kucha zake zilikuwa zinebadilika ranging Imekuwa dark blue.

Ameendelea kudai kuwa katika uchunguzi wake wa sehemu za ndani za mwili wa marehemu waligundua kuwa pingili mbili za shingo ya marehemu  zilikiwa zimetenguka na kulikuwa na kulikuwa na mvililio wa damu kuzunguka hizo pingili na pia mapafu yake yalikuwa yamejaa hewa na damu.
" katika uchunguzi wangu nilibaini kuwa majeraha kwenye shingo ya marehemu ndio chanzo cha kifo chake", amedai Dr. Mosha.

Kufuatia ushahidi huo, Mahakama imemkuta mshtakiwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kufungua ushahidi dhidi ya kesi hiyo kwa kuleta mashahidi sita.

Wiki iliyopita, watoto wawili wa marehemu akiwemo mtoto wa miaka 10, ambae wakati mama yake anauwawa alikuwa na miaka mitano alitoa ushahidi wake na kueleza alivyoshuhudia  baba yao wa kambo, Godfrey Samweli au Nkwabi (mshtakiwa)akimnyonga mama yake Bahati Hussein.

Inadaiwa Juni 21, 2014 huko Ulongoni A wilayani Ilala, Dar es Salaam, Godfrey alimuua kwa makusudi Bahati  Hussein.
Mshtakiwa Godfrey Samwel maarufu Nkwabi akitoka ukumbi wa wazi wa  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi yake ambapo leo Shahidi wa sita ambae ni daktari bingwa wa uchunguzi wa vifo vyenye utata na magonjwa mbali mbali ametoa ushahidi wake.
Hata hivyo, upande wa mashtaka umemkuta mshtakiwa huyo na kesi ya kujibu na kesi imeahirishwa hadi Julai 18 mshtakiwa atakapoanza kujitetea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...