Na Abdulatif Yunus, Michuzi TV, Bukoba

Hatimaye Msanii nguli nchini Diamond Platinum akiambatana na Wasanii wenzake ambao wapo chini ya Kampuni (Lebal) ya WASAFI wawasili mkoani Kagera na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti tayari kwa uzinduzi wa Tamasha kubwa la (WASAFI FESTIVAL) Wilayani Muleba Julai 19, 2019.

Mara baada ya kuwasili ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa Gaguti  alimpongeza Diamond na uongozi wa WASAFI kwa kuamua Tamasha la Wasafi lianzie katika Mkoa wa Kagera pia kushirikiana na TACAIDS kuhakikisha wanawahamasisha vijana kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI, kutumia kinga pia kutumia dawa kwa wale ambao tayari wameambukizwa na VVU>

“Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kimkakati ni rahisi sana kwenda Kigali, Kampala na Buumbura kutokea hapa Bukoba kuliko kwenda Singida hapa ni karibu sana na nchi jirani kwa hiyo kuleta WASAFI FESTIVAL pia nchi jirani zinanufaika kwa wapenda burudani kuja kuona wasanii wakubwa hapa kwetu Kagera” Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wasanii hao kushiriki katika wiki ya uwekezaji Kagera ambayo inatarajia kuanza Agosti 12 hadi 17, 2019 na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Naye Msanii Diamond Platinum alimshukuru Mkuu wa Mkoa Gaguti kwa kukubali kuwapokea pia kuonesha ushirikiano katika mkoa wake wa Kagera. Diamond alisema kuwa yeye na wasanii wenzake ni vijana na wanajua ni namna gani ya kuongea na vijana wenzao kwa kuwahamasisha kujikinga na maambukizi mapya ya Virus vya UKIMWI na ndiyo maana wanashirikiana na TACAIDS kutoa elimu hiyo.

Said Fella Meneja wa Msanii Diamond alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa mapokezi lakini pia alisema kuwa kuleta Tamasha la Wasafi Mkoani Kagera ni fursa kwa vijana Bodaboda, mama lishe, wamiliki wa Hoteli na wafanyabiashara mbalimbali. “Sisi timu yetu tumekuja zaidi ya watu mia moja kwahiyo ni fursa hiyo.” Aliongeza Said Fella.

Msanii Diamond Plutnum amewasili mkoani Kagera Julai 18, 2019 na ameambatana na wasanii wenzake Rayvany, Malomboso, Queen Darlin, Rubi, Dulla Makabira, na wengineo na Tamasha la WASAFI linatarajiwa kuzinduliwa rasmi nchini Wilayani Muleba Ijumaa Julai 19, 2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...