Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MHADHIRI Wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samsoni Mahimbo (68), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali kutoka Takukuru Vera Ndeoya amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi amedai, mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 12 , 2017 huko katika nyumba ya kulala wageni ya  Camp David  iliyoko Mlalakuwa Mwenge.

Imedaiwa, Siku ya tukio, mshtakiwa akiwa  muajiriwa wa chuo hicho cha NIT kama mhadhiri kwa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/2016 wa somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji (road transport management), lenye kodi namba 07101 alitumia mamlaka yake kutokana na nafasi yake chuoni hapo na kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi, Victoria Faustine ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho  anayosomea mafunzo hayo ya road transport management.

Imeendelea kudaiwa kuwa, mshtakiwa aliomba rushwa hiyo kama sharti kwa mwanafunzi huyo kuwa atamfaulisha katika mtihani wa marudio (Supplement) wa somo hilo  uliokuwa ukifanyika January 5, 2017.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo Mahakama ilimtaka kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya sh. Milioni nne

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Septemba 17,2019 mshtakiwa atakaposomewa Maelezo ya awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...