Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha imepanga kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 20.7 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya ndani.

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mkurugenzi wa jiji hilo,Dkt Maulid Madeni amesema kuwa licha ya jiji hilo kuvuka malengo ya makusanyo mwaka wa fedha 2019/20 na kushika Namba moja kwa majiji yote nchini,amesema mpango wa jiji hilo ni kufikia makusanyo yanayozidi sh, milioni 30 kwa mwaka .

Dkt Madeni amesema kuwa pamoja na pongezi nyingi alizopata za kuvuka makusanyo ya ndani, amesema kipaumbele chake si kupongezwa na wala hapokei pongezi hizo bali ni kufikia malengo ya makusanyo aliyojiwekea .

"Mimi si mtu wa kusifiwa na wala sikubali pongezi hizo ninachotaka bado hakijafikiwa, lengo langu ni kufikia makusanyo ya bilioni 30 " Amesema Madeni.Katika hatua nyingine Dkt Madeni amesema kuwa jiji la Arusha limetenga bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi na ukumbi wa Mkutano.

Dkt Madeni amesema ujenzi wa jengo hilo unatarajia kuanza mapema mwaka wa fedha 2919/20 na litajengwa jirani na ofisi za sasa za halmashauri hiyo.

Pia Mkurugenzi huyo amedai kuwa jiji la Arusha limetoa kiasi cha shilingi milioni 140 kwa wakala wa barabara za mijini na vijiiini Tarura kwa ajali ya kuzifanyia ukarabati barabara zote za jiji hilo zilizoharibiwa na mvua kipindi cha masika.

Amesema barabara hizo zitafanyiwa matengenezo na kuondoa malalamiko yanayojitokeza kwa watumiaji wa barabara wakiwemo watumiaji wa vyombo vya moto ambao wamekuwa wakilalamika kuharibika kwa magari yao kutokana na mashimo yaliyopo.

Wakati huo huo jiji hilo limesaini mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 3.5 itakayojengwa kwa kiwango cha Lami kwa thamani ya shilingi bilioni 4.1.

Akiongea wakati wa kusaini mkataba huo baina ya jiji hilo na kampuni ya ujenzi ya Sinohydro kutoka nchini china Meya wa jiji la Arusha, Kalist Lazaro alisema kuwa mradio huo ni kazi ya nyongeza ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Kisongo Bypass inayotoka Olasiti jijini hapa.

Meya alisema kuwa mkandarasi huyo atafanyakazi yenye ubora kwa muda wa miezi minne kuanzia September 11/2019/hadi January 11/2020 atakapokabidhi mradi huo.
Mkurugenzi wa jiji hilo,Dkt Maulid Madeni Wa kwanza kushoto akimkabidhi mkataba huo waluisaini baina ya jiji hilo na kampuni ya ujenzi ya Sinohydro kutoka nchini china.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...