Karama Kenyunko

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Agosti 23 mwaka huu kusikiliza maombi ya chini ya hati ya dharura ya kutoa amri ya kusitisha mchakato wa kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) yaliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu.

Maombi ya Lissu namba 18 ya mwaka 2019 yametajwa jana mahakamani hapo mbele ya Jaji Sirilius Matupa ambapo Lissu anawakilishwa na jopo la Mawakili wanne akiwemo Peter Kibatala, huku upande wa Serikali ambao ni wajibu maombi ukiwakilishwa na mawakili wanne akiwemo Wakili wa Serikali Mkuu, Vincent Tango.

Hatua hiyo imefikwa leo Agosti 15, 2019 baada ya Wakili Kibatala kuwasilisha ombi la kuitaka mahakama itoe amri ya kusitisha kuapishwa kwa mbunge mteule Mataturu, Wakili wa Lissu ambaye ni Kibatala aliomba mwongozo wa mahakama ili waweze kuzungumzia suala hilo la kusimamishwa kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, lakini ombi hilo likapingwa na mawakili wa Serikali wakidai kuwa kwa sasa sio muda sahihi wa kuanza kulisikiliza jambo hilo. 

Pia upande wa wajibu maombi waliomba muda wa siku nane ili waweze kuwasilisha hati ya kiapo kinzani pamoja na hati ya maelezo kinzani kabla ya maombi hayo kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa.

Wakili wa Serikali Mkuu, Tango alidai wanaomba siku hizo kwa kuwa shauri hilo linahusisha mhimili mwingine, yaani Bunge hivyo wanahitaji kupata muda wa kushauriana na Bunge (Spika) ili kuweza kuandaa kiapo kinzani.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sirilius Matyupa alisema atatoa uamuzi wa kusitisha mchakato wa kuapishwa kwa mbunge huyo mteule Mtaturu baada ya kusikiliza maombi yote ya Lissu, Agosti 23, mwaka huu.

Katika maombi yake, Lissu anaiomba Mahakama kumwamuru Spika wa Bunge Job Ndugai awasilishe mahakamani taarifa ya kumvua Ubunge aliyoitoa bungeni ili iweze kupitia na kisha iamuru kuutengua na kuutupilia mbali. 

Pia anaomba Mahakama imwamuru Spika ampatie yeye Lissu nakala ya taarifa ya kumvua ubunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...