Na Leandra Gabriel Michuzi TV

RAIS wa Awamu tatu Benjamin William Mkapa amesema nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zina amani ya kutosha huku akitumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo marais wa nchi za jumuiya hiyo wamekuwa wamoja katika kutatua changamoto mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi.

Amesema kuwa changamoto zinazoikumba jumuiya hiyo ni pamoja na masoko, umaskini, kiwango kidogo Cha uwekezaji,kiwango duni cha teknolojia na changamoto ya miundombinu rafiki ndani ya jumuiya ni mambo yanayotakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuweza kuendana na dhima ya jumuiya hiyo ambayo daima imejikita katika kuhakikisha uchumi, uzalishaji, utawala Bora amani na ulinzi vinapewa kipaumbele zaidi.

Akiwa amestaafu katika nafasi hiyo ya uenyekiti wa kwa miaka 14 Sasa Mkapa amesema kuwa Kuna mambo lazima yawekewe mkazo na hayo ni pamoja na kuongeza uzalishaji katika nchi wanajumuiya, viwanda ambavyo vitakakata bidhaa zinazozalishwa, uwekezaji pamoja na teknolojia ili kuweka ushindani katika soko la kimataifa.

Aidha amezishauri nchi wanachama kutengeneza ajira nyingi zaidi hasa kwa kundi la vijana na hiyo ni pamoja na kuweka mifumo rafiki ya elimu ambayo itawapa maarifa ya kutengeneza ajira zao wenyewe na sio kutegemea kuajiriwa pekee na amezitaka taasisi za sekta binafsi na serika kushirikiana katika kutatua changamoto za kiuchumi ili kuweza kujenga uchumi imara ndani ya jumuiya.

Vilevile ameshauri masuala Kama uwekezaji wa vikwazo vya biashara havina budi kuondolewa na kuweka masoko ya uhakika na hiyo ikienda sambamba na kutumia bidhaa ndani ya jumuiya hiyo hali itakayochochea ukuaji wa kasi wa uchumi unaojitegemea kwa nchi wanachama.

Hata hivyo Mkapa amesema kuwa mlengo wa jumuiya ya SADC ni kuleta mapinduzi hasa ya kiviwanda hivyo jumuiya haina shida budi kutoa maarifa na ujuzi kwa vijana ili waweze kuleta mabadiliko hasa ya kiteknolojia yatakayoleta ushindani katika soko la kimataifa na teknolojia hiyo ni kwa kuzingatia uwepo wa uimara katika masuala ya miundombinu, nishati na viwanda.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa akihutubia katika mhadhara uliofanyika  leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,uliohusu historia ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...