Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Januari mwaka jana alivitangazia vyama vyote vya siasi nchini kuhusu kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Ofisa Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni, Victoria Wihenge ameeleza hayo leo Agosti 21,2019 wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, Wihege ambaye ni shahidi wa sita wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo amedai, taarifa ya tume ilielekeza kwamba uchaguzi huo unapaswa kufanyika Februari 17, 2018.

Amedai, baada ya taarifa hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi manispaa hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni aliitisha kikao cha wadau wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini.

Na kwamba jumla ya vyama vya siasa 19 vikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa Wilaya vilishiriki katika kikao hicho ambacho lengo lake lilikuwa ni kuwajulisha tarehe ya uchaguzi, siku ya kufanya uteuzi wa wagombea ubunge na kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.

"Miongoni mwa vyama vilivyoshiriki katika kikao hicho ni Chadema, CCM, Ada Thadea, AFP, CUF, UND, Demokrasia Makini, TLP na NRA. Viongozi wa vyama hivi tuliwataarifu kuhusu uwepo wa uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kinondoni na ushiriki wao katika kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika," alidai Wihenge.

Ameendelea kudai kuwa, baada ya kikao hicho wajumbe walienda kufanya maandalizi ya kuchukua fomu na uteuzi ambapo fomu zilianza kuchukuliwa Januari 14 hadi Januari 20,2018 ambapo kila chama kilitakiwa kupeleka jina la mgombea mmoja wa ajili ya kulipeleka katika kamati ya maadili na kamati ya kampeni.

Aidha alitaja mambo ya kuzingatia katika uchaguzi ikiwamo kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na katiba kuanzia tarehe ya kutangazwa uchaguzi hadi kufanyika kwa uchaguzi.

Mapema akimalizia kutoa ushahidi wake, shahidi wa sita Koplo Charles amedai alipangiwa na bosi wake kuripoti mkutano wa kufunga kampeni jimbo la Kinondoni na kwamba katika video iliyooneshwa mahakamani hapo haikuwa na tarehe kwa sababu hakuseti kamera yake ionyeshe vitu hivyo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori shahidi huyo ameendelea kudai kuwa alishindwa kuendelea kurekodi matukio katika mkutano huo wa Chadema kutokana na kauli vya viongozi hao ambazo zilikuwa zinatishia amani.

Alidia hakukuwa na kibao wala alama ya utambuzi, na kwamba yeye alienda pale kwa ajili ya kuchukua matukio ya mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chadema.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...