*Puma nao wampongeza Rais kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji

 Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imemueleza Rais Dk.John Magufuli kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji nchini yameifanya kampuni hiyo kuendelea kutengeneza faida mwaka hadi mwaka na hivyo imesababisha kuongezeka kwa gawio kwa Serikali.

Rais Magufuli alifika kwenye banda la Puma Energy Tanzania wakati anatembelea mabanda katika Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) yanayoendelea Ukumbi wa  Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la Puma Energy Tanzania, Rais Magufuli pamoja na mambo mengine aliuliza maofisa wa kampuni hiyo mwaka huu wamejipanga kutoa gawio la shilingi ngaoi kwa Serikali, ambapo alijibiwa watatoa Sh.bilioni 22 ambapo  Sh.bilioni 11 zitakwenda kwa Serikali.

 "Mwaka jana mlitoa gawio kiasi gani?(Akajibiwa) basi mwaka huu uongezeni  ongezeni kidogo,"alisema Rais Magufuli ambapo maofisa wa Puma nao  wakamhakikishia Rais kuwa watajitajihidi kuongeza huku wakipongeza mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yamesababisha wao kuendelea kufanya vema siku hadi siku.

Akizungumza mbele ya Rais Meneja Operesheni wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Lamecky Hiliyai amemwambia Rais kuwa kampuni hiyo kutokana na mazingira mazuri yaliyopo nchini katika uwekezaji wamekuwa wakiendelea kufanya biashara ya mafuta na kupata faida.

"Mheshmiwa Rais tunashukuru kwani kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji katika nchi yetu, nasi Kampuni ya Puma tumeendelea kufanya biashara, hivyo tumeendelea kupata faida na tunaahidi hata gawio kwa Serikali nalo tutaendelea kuongeza mwaka hadi mwaka,"alisema Hiliyai.

Kwa upande wake Meneja wa Sheria na Mahusiano ya kampuni hiyo, Godluck  Shirima amewaambia waandishi wa habari Kampuni yao inajivunia kufanya 

biashara katika nchi 13 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Kampuni hiyo ambayo inamilikiwa kwa ubia na Serikali ya Tanzania imesema  mbali na kudhamini maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC pia imekuwa ikisaidia  jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Shirima, alisema wamekuwa wakijiendesha kwa faida tangu walipoanza shughuli  zao mwaka 2011/12. Kwa mujibu wa Shirima mwaka 2011/12 walitoa gawio la Sh bilioni 3.5 kwa wanahisa wake na kati ya fedha gizo Serikali ilipata Sh bilioni 1.25.

Alisema mwaka 2018/19 wanatarajia kutoa gawio la Sh bilioni 22 na Serikali  itapata Sh bilioni 11. "Sisi ni wadau wakubwa wa SADC ndio maana tumedhamini maonesho haya na shughuli zingine za mikutano na tuko hapa kuonesha bidhaa  na huduma zetu kwa nchi wanachama," alisema Shirima.

Ameongeza hata katika uwekezaji unaofanywa na Serikali hasa katika ujenzi wa miundombinu wa kuwezesha usafirishaji wa malighafi na rasilimali za viwanda  umeiwezesha kampuni hiyo kuendelea kunufaika.

"Tumekuwa tukisambaza mafuta katika miradi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa 
(SGR), Daraja la Salenda na tumejenga mfumo wa usafirishaji mafuta katika 
jengo la tatu la abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,"amesema Shirima.
Rais Dk.John Magufuli akipata maelezo katika Banda la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania akipata maelezo kutoka kwa Meneja Opereheni Lamecky Hiliyai kuhusu namna  ambavyo wanaonesha shughuli zao.Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuwataka Puma kuendelea kuongeza gawio kwa Serikali ambapo maofisa wa Puma wamemhakikishia kutekeleza maagizo yake.Wa kwanza kushoto ni Meneja Sheria na Mahusiano wa kampuni hiyo Godluck Shirima.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma  EnerTanzania,alipotembelea banda hilo katika wiki ya maonesho ya Biashara kwa nchi za SADC yanayoendelea jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...